WAREMBO 12 wanaotarajia kuwania taji la kitongoji cha Kigamboni mwaka
huu 'Miss Kigamboni City 2012' leo Jumatano wanatarajiwa kufanyiwa
usaili kwa ajili ya kuanza safari ya kumpata mshindi wa shindano hilo
litakalofanyika Ijumaa kwenye ukumbi wa Navy Beach jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa shindano hilo, kutoka kampuni ya K&L Media Solutions,
Somoe Ng'itu, alisema jana kuwa maandalizi ya zoezi hilo yamekamilika na
wanachosubiri ni siku ya shindano ifike.
Alisema kuwa kitongoji hicho kina warembo wenye sifa na wanaojiamini
ambao wamepania kurudisha taji la Miss Tanzania kwenye Kanda ya Temeke.
Aliongeza kuwa ili kuboresha shindano hilo bendi ya muziki wa dansi ya
FM Academia maarufu Wazee wa Ngwasuma na msanii na mchekeshaji mahiri
hapa nchini, Mpoki watatumbuiza kwenye kinyang'anyiro hicho.
"Tunawaomba wadau wa sanaa ya urembo kufika kushuhudia mrembo wa
Kigamboni atakavyopatikana, ni Kitongoji kilichoko sehemu pekee hapa
nchini na kulikosa kushuhudia itakuwa ni kujinyima burudani wewe
mwenyewe," alisema mratibu huyo.
Aliwataja warembo watakaochuana kuwa ni pamoja na Susanne Jeremiah,
Agness Goodluck, Elizabeth Boniface, Dorothea Kessy, Esther Albert, Edda
Silyvester, Sophia Martin, Doreen Kweka, Khadija Kombo, Linnah David,
Rosemary Peter na Winnie Karaya.
Aliwashukuru wadhamini ambao wamejitokeza kusaidia shindano hilo ambao
ni Redd's, Dodoma Wine, hoteli ya Hope Country, Screen Masters, Global
Publishers, Nobro Collections, Times FM na Clouds FM.
Aliongeza kuwa warembo watakaoshika nafasi tatu za juu kutoka katika
shindano hilo wataungana na wenzao kutoka vitongoji vya Kurasini na
Chang'ombe ili kuwania taji la Kanda ya Temeke baadaye mwaka huu.
PUBLIC RELATION SPORTS.
This Blog deals with sports and games at SAUT.
Tuesday, June 12, 2012
MESSI AWAFUNDISHA SOKA WABRAZIL: APIGA HAT TRICK ARGENTINA WAKIUA BRAZIL 4-3
Thursday, June 7, 2012
WENDAWAZIMU WANAONGOZA KWA USHAMBULIAJI LIGI YA ITALY
Maneno ya
Cesare Prandelli alipomrithi Marcello Lippi kama kocha wa timu ya taifa
baada ya kombe la dunia mwaka 2010 ni kwamba ataifanya Azzuri ivutiwa
kwa kucheza soka zuri la kushambulia. Kwa hakika amejitahidi sana huku
akitambulisha utaratibu wa 'ethical code' (wachezaji wanaokuwa
wamesimamishwa kwa makosa ya kinidhamu hawatoitwa timu ya taifa) na
kusisitiza katika kuwapa nafasi zaidi viungo wenye ufundi zaidi katika
timu yake. Wazo ni kuifanya Italia kucheza kwa staili yake ya mfumo wa
tiki-taka, staili inayopendelewa zaidi na Wahispania.
Akiuacha mfumo wa siku nyingi wa kujenga ukuta wa chuma na kucheza kwa mashambulizi ya kushtukiza kwa ajili ya mfumo ambao unatumia na Spain, ambao mpaka sasa umeleta matokeo ya mchanganyiko. italy haikufungwa hata mechi moja kwenye hatua ya kufuzu, lakini wamekuwa wakifungwa kwenye mechi za kirafiki. Skendo ya upangaji wa matokeo ambayo inaliandama soka la nchi hiyo kwa miaka mingi sasa, haitegemewi kuwa na madhara makubwa sasa hivi kuliko ilivyokuwa katika miaka 1982 na 2006, sababu kubwa ni kwa kuwa ni wachezaji wachache wa kikosi cha sasa wameguswa na kashfa hiyo, lakini suala hilo bado linabakia kuwa sio zuri kwa wachezaji.
Droo ya group C haikuwa nzuri kwa Italy, lakini atleast mechi yao dhidi ya Spain itakuwa ya kwanza. Na kupata pointi kutoka kwenye mechi hiyo ni jambo ambalo linawezekana, kwa kuangalia Spain huwa na kawaida ya kuanza vibaya michuano mikubwa, ukiangalia kombe la dunia lilopita walipofungwa na Uswis katika mechi ya kwanza makundi. Baada ya mechi hiyo atleast kidogo mambo yanaweza kuwa mazuri dhidi ya Croatia na Ireland.
WACHEZAJI MUHIMU
Gianluigi Buffon
Nahodha amerudi kwenye kiwango chake baada ya majeruhi yaliyomkumba msimu wa 2010-11. Ukifikiria namna safu ya ulinzi ilivyokuwa dhaifu, Azzuri wanahitaji kuwa na Buffon mwenye kiwango cha juu ili kuepeuka balaa. Ni uchizi sasa kufikiri kwamba safu ya ulinzi ambayo siku zote imekuwa ndio nguzo ya timu ya taifa ya Italia, sasa hivi ndio ulipo udhaifu wao, lakini hapa ndipo tulipo, na sasa tumaini lote lipo kwa Buffon na mikono pamoja na miguu yake kutatua hilo tatizo.
Mario Balotelli
Mario Balotelli alisema hatoshangilia goli mpaka atakapofunga goli la ushindi kwenye world cup au Euro, hivyo hii ndio nafasi pekee kumuona Super Mario akicheza kwa furaha baada ya kutupia kambani. Tuache utani, huu ni muda wake kuweza kuonyesha kwanini makocha wamuamini na kumpa nafasi. Balotelli ana nguvu, ujuzi na kimo kizuri, Anachohitaji ni kutulia na kutumia vizuri nafasi atakazopata huku akijiepusha na suala la nidhamu mbovu. Akifanikiwa kwenye hayo atatisha.
Daniele De Rossi
Katika kiungo ambacho kimejaa wapiga pasi mafundi zaidi, De Rossi ndio kiumbe anayetegemewa kusambaza minguvu yake. Shujaa huyu wa Roma ndio sasa anaelekea kwenye kilele chake, akiwa ameshaji-commit kwenye klabu yake, sasa yupo huru kufikiria timu ya taifa tu. Atakuwa na shughuli ngumu katika kupambana na kuizuia safu ya ulizni wa timu ambayo ni dhaifu kutoguswa

JE SAFU YA USHAMBULIAJI YA MACHIZI ITAFANYA VIZURI?
Mara tu Giueseppe Rossi alipoumia, mikono ya Prandelli ilikuwa imefungwa. Akawa hana chaguo lingine zaidi ya kuwatumia Balotelli na Antonio Cassano. Hii haihusu suala la uwezo - -wachezaji wote wawili wana vipaji vikubwa tataizo ni nidhamu: wote wawili wana matukio mengi ambayo yanahusu ukosefu wa nidhamu na tabia nyingine tofauti,ndani na nje ya uwanja. Hivyo hilo ni tatizo ambalo Prandelli inabidi alitafutie suluhisho.
YANGA NA SIMBA MAMA YAO NI MMOJA
Kikubwa zaidi ninachojaribu kukiangalia ni jinsi ambavyo viongozi wa vilabu vya SIMBA na YANGA wasivyopenda kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa, mwenyekiti wa SIMBA ameongelea kwa jazba kubwa sakata la beki wa timu yake Kelvin Yondani kusajiliwa na Yanga, si ajabu kesho tu tukasikia viongozi wa YANGA nao wakilijibu hili kwa mbwembwe.
Lakini mwisho wa siku ni lazima tukubali kuwa viongozi wote hawa wa simba na yanga wana mapungufu makubwa sana katika utendaji wao wa Kazi, na namna wanavyoendesha vilabu vyao na mpira wa Tanzania kwa ujumla.
Viongozi hawa wa SIMBA na YANGA Wamekuwa wakifanya mambo mengi sana ya ajabu ajabu. SIMBA na YANGA ni vilabu ambavyo vinatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na vilabu vingine vidogo hapa nchini.
Lakini kwa mambo ambayo yamekuwa yakifanyika ndani ya vilabu hivi vikubwa ni ya ajabu sana na ya kusikitisha mno.
Kwa sakata hili la KELVIN YONDANI kumekuwepo na watu ambao wamekuwa wakijaribu kumshutumu mchezaji huyo, lakini mimi binafsi siwezi kumshutumu hata kidogo kwanza, hatujui wakati anasainishwa mkataba na Yanga alikuwa katika mazingira gani labda alitekwa na kulazimishwa,
Pili, labda aliamua tu kusajili huku akisema liwalo na liwe hao Simba wenyewe wamenisainisha mkataba kwa 'mkopo' wakati Yanga wamekuja mezani na mipesa yote hii.
Tatu, kusukumwa na hisia za kukumbuka manyanyaso yasiyoisha ya kushutumiwa kufungisha, mara ugomvi na baadhi ya viongozi Simba.Nne, kutokutambua umuhimu na kuuheshimu mkataba wake na Simba.
Kwa nchi za wenzetu zilizoendelea kitendo cha mchezaji kusaini mkataba ni kitu muhimu mno, lakini huku kwetu umuhimu na thamani ya mkataba hujulikana wakati wa matatizo hasa pale tu mchezaji anapotaka kuondoka na kwenda kujiunga na klabu nyingine.
Mimi nina uhakika wa zaidi ya asilimia mia moja kwamba hakuna mchezaji anayechukua mkataba na kuusoma, kuuelewa vipengele vilivyomo kabla ya kuusaini.
Ninachojua ni kwamba mchezaji huwa anaangalia napata kiasi gani…nazungumza hili kwasababu nina uhakika nalo na lilishawahi kunitokea wakati nacheza mpira, wakishakubaliana anaonyeshwa pakuweka saini na dole gumba kisha anachukua mzigo wake na kusepa.
Ndio maana wenzetu huwa wanawatanguliza wawakilishi, mchezaji anapokwenda kusaini mkataba ni lazima kuwa na meneja/wakala ama mwanasheria wake, lakini hapa kwetu Tanzania ni kinyume kabisa,wachezaji wenyewe hata darasa la saba hawajamaliza halafu anaenda kusaini mkataba tena wa kisheria tena ulioandikwa kwa lugha ya kiingereza, je ana uwezo wa kuelewa? au tunadanganyana tu na kupotezeana muda.
Professionalism inatakiwa kuanzia kwa viongozi wa vilabu kabla ya wachezaji, kwa maana viongozi wanatakiwa kusimamia sheria kama zilivyo, lakini cha kustaajabisha viongozi hao hao wa vilabu ndio wanakuwa vinara kwa kupindisha sheria hizo na kushindwa kwenda nazo sambamba.
Hivyo inapotokea ishu kama hii ya leo pasipo kufuata uweledi ndipo mmoja anaonekana kuonewa au kwenda against na mwenzake lakini kumbe wote wana makosa makubwa.
Ina maana hawa viongozi wanaowasainisha hiyo mikataba ya kisheria hao wachezaji hawajui kama hawana elimu ya kutosha ya kuisoma na kuielewa hiyo mikataba jamani hii lugha ya kiingereza inayotumika kwenye hii mikataba (mimi mwenyewe inaniacha ) ni mchezaji gani wa kitanzania mwenye uwezo wa kuisoma na kuielewa kabla ya kusaini na kuweka dole gumba? kama kweli hawa viongozi wanawatakia mema hawa wachezaji kwanini hiyo mikataba isiwekwe kwenye lugha ya Kiswahili angalau wanaweza kuambulia kitu. ( au kisheria ni lazima mkataba uwe kwenye lugha ya kiingereza ?)
Ishu kama hii ya YONDANI bila kuhangaika sana ebu tuangalie KANUNI ZA USAJILI zinasemaje
Kanuni ya 57
Uhamisho wa mchezaji
(1) Kilabu inaweza kumhamisha mchezaji kutoka kilabu kimoja hadi kingine, kwa madhumuni ya kumsajili, baada ya ligi kumalizika, au katika kipindi cha usajili wa katikati ya msimu. Kilabu inayotaka kumsajili mchezaji aliyesajiliwa na kilabu kingine au mwenye mkataba na kilabu kingine, italazimika kuafikiana na kilabu yake kabla ya kumsajili mchezaji huyo. Hata hivyo kilabu ambayo itaruhusiwa kusajili mchezaji katikati ya msimu ni ile ambayo haijatimiza wachezaji thelathini (30) au ile ambayo imempa mchezaji wake ITC ya kwenda kucheza soka nje ya nchi, au ile ambayo mchezaji wake amehamia kilabu kingine cha ndani kwa mujibu wa kanuni hii.
Kanuni ya 45
Usajili na uhamisho wa wachezaji
(4) Mchezaji ana uhuru wa kujisajili na kilabu kingine katika msimu mmoja iwapo kutakuwa na maelewano kati ya kilabu yake na ile inayotaka kumsajili.
(5) Kilabu inawajibika kuingia mkataba na mchezaji wa kuichezea lakini mkataba huo ni lazima uthibitishwe na TFF. Ada ya kuthibitisha mkataba ni shilingi elfu hamsini (50,000/=).
(6) Mchezaji ambaye ameingia mkataba wa zaidi ya msimu mmoja hatoruhusiwa kujisajili na kilabu kingine kabla ya kilabu yake mpya kuafikiana na kilabu yake ya zamani.
Kanuni ya 56
Katazo
Haitaruhusiwa kwa mchezaji yeyote kutia saini kwenye mikataba wa vilabu viwili tofauti kwa wakati mmoja na inayohusu kipindi kimoja. Mchezaji atakayesaini mikataba ya timu mbili tofauti kwa wakati mmoja, ataadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 44 (4) ya kanuni hizi.
Kutokana na vipengele hivyo hapo juu hakuna mchezaji ambaye anaweza kuhama timu moja kwenda timu nyingine kihuni huni tu pasipo kufuata kanuni na taratibu.
Sakata la Simba na Azam juu ya usajili wa Ibrahim Jeba.
Lazima tusiwe wanafiki, waswalihi wanasema mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu mchungu, wakati tukiwa tunalijadili sakata hili la Yondani si vibaya pia tukaliwe mezani sakata linalomuhusu mchezaji Ibrahim Jeba aliyesajiliwa na Simba Kutoka Azam pasipo taratibu kufuatwa.
Kanuni ya 44
Masharti ya mikataba kati ya wachezaji na kilabu
(1) Muda wa chini wa mkataba utakuwa kuanzia tarehe ya kuanza kutumika hadi mwisho wa msimu. Muda wa juu wa mkataba utakuwa ni kipindi cha miaka mitano (5). Mikataba ya muda mwingine wowote itakubaliwa kama inafuata Sheria ya Mikataba inavyosema. Mchezaji chini ya umri wa miaka 18 haruhusiwi kuingia kwenye mkataba wa mchezaji wa kulipwa kwa kipindi kinachozidi miaka mitatu (3), sharti lolote linalotaja kipindi kirefu zaidi halitatambuliwa.
(2) Kilabu inayotarajia kuingia mkataba na mchezaji wa kulipwa haina budi kuiarifu kilabu yake ya sasa kwa maandishi kabla ya kufanya makubaliano na mchezaji huyo wa kulipwa. Mchezaji wa kulipwa atakuwa huru tu kuingia mkataba na kilabu nyingine iwapo mkataba wake na kilabu yake ya sasa umekwisha au utakwisha baada ya miezi sita (6). Uvunjaji wowote wa sharti hili utastahili vikwazo vinavyofaa.
Niliposema viongozi wote hasa wa vilabu vya SIMBA na YANGA ndo wenye matatizo makubwa nilikua namaanisha vitendo kama hivi.
Kufanya mazungumzo ya siri na mchezaji pasipo kupata ruhusa ya klabu yake ni kosa kubwa ambalo hata FIFA wanalipiga vita.
Ina maana Kulwa na Doto hawazijui hizi taratibu na kanuni za kusajili mchezaji ?
Wednesday, June 6, 2012
YANGA YATANGAZA KUMSAJILI KEVIN YONDAN HUKU SIMBA IKIMUONGEZEA MKATABA KELVIN YONDANI.
Leo hii klabu ya Yanga imetangaza kumsajili kinda raia wa Tanzania Kevin Patrick Yondan
mwenye umri wa miaka 17,Yondan ambaye anacheza nafasi ya beki wa kati
hajajulikana ametokea Klabu gani alizaliwa 9/10/1994.Mkataba wa Yanga na
kinda huyo ni wa miaka miwili na unataraji kumalizika msimu wa
2013/2014.
hapa chini ni sehemu ya mkataba wa beki huyo na klabu ya Yanga yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani.
Mchezaji Kelvin Yondani akisaini mkataba wa usajili mbele ya kiongozi wa Yanga Seif Ahmed usiku huu, katika picha hii Yondani anaonekana akiwa amevaa fulana na timu ya taifa ambazo zimeanza kutumika mwezi mmoja uliopita baada ya stars kuingia mkataba na TBL KUPITIAKilimanjaro.
Taarifa nilizozipata hivi punde Yondani amefuatwa kwenye kambi ya timu ya Taifa iliyopo kwenye Hotel ya Tansoma jijini Dar Es Salaam.

Wakati huo huo Simba Sc imetangaza kumuongezea mkataba wa miaka miwili beki wake wa kati Kelvin Patrick Yondani, mkataba huo mpya ulisainiwa tangia mnamo 23/12/2011 ikiwa ni maboresho ya mkataba wa awali uliokua unafika kikomo mwishoni mwa mwezi uliopita yaani 31/05/2012. Yondani mwenye umri wa miaka 27 pia ni beki wa kimataifa wa Tanzania.
Kelvin Patrick Yondani
![]() |
|
Baadhi ya michezo ambayo Kelvin Patrick Yondani ameichezea timu ya Taifa ya Tanzania.
Tarehe | Nyumbani | matokeo | Ugenini | ||
---|---|---|---|---|---|
2012-06-02 | Côte d'Ivoire |
2 - 0
| Tanzania | ||
2012-05-26 | Tanzania |
0 - 0
| Malawi | ||
2012-02-23 | Tanzania |
0 - 0
| Congo DR | ||
2011-11-15 | Tanzania |
0 - 1
| Chad | ||
2011-11-11 | Chad |
1 - 2
| Tanzania | ||
2010-06-07 | Tanzania |
1 - 5
| Brazil | ||
2010-01-04 | Tanzania |
0 - 1
| Côte d'Ivoire |
WEKUNDU WA MSIMBAZI:
SIMBA YAKAMILISHA USAJILI WA SALUM KINJE WA AFC LEOPARDS:
Taarifa rasmi za uhakika kutoka ndani ya uongozi na kamati ya ufundi ya klabu ya Simba ni kwamba timu hiyo imefanikiwa kukamilisha usajili wa mchezaji bora wa nafasi ya kiungo kwenye ligi kuu ya soka nchini Kenya, Salum Kinje ambaye anaichezea AFC Leopards.
Kinje ambaye ni mtanzania amesajiliwa na Simba kwa kiasi cha fedha ambacho hakijawekwa wazi na pande zote mbili, lakini amesaini mkataba wa kuitumikia Simba kwa miaka 2 na siku chache zijazo ataanza mazoezi na timu yake mpya inayojiandaa kushiriki michuano ya Kagame Cup inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
UFARANSA:
TIMU YA UFARANSA HAIJASHINDA MECHI YOYOTE KWENYE EURO WALA WORLD CUP TANGU 2006: ITAFANYA NINI KWENYE EURO 2012.
Laurent Blanc anaichukua Ufaransa
kwenda nayo kwenye Euro 2012 huku akiiongoza timu hiyo kutofungwa katika
michezo 20, ambayo inahusisha ushindi dhidi ya Ujerumani, England na
Brazil. Lakini kocha huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa bado haipi nafasi
kubwa timu. Ufaransa haijashinda mechi yoyote ya mwisho ya michuano
mikubwa yenyewe tangu mechi ya nusu fainali ya World Cup 2006
(haikushinda mechi yoyote kwenye Euro 2008 na WOZA 2010), huku wakishika
nafasi ya 16, nafasi tisa nyuma ya wapinzani wao England wanaoshika
nafasi ya saba kwenye ubora wa viwango wa FIFA.
Blanc bado na maumivu ya kichwa kuhusu upangaji wa kikosi hasa kwenye nafasi ya beki wa kushoto, ambapo Gael Clichy ameonyesha kiwango kizuri kwenye mchi dhidi ya Serbia siku chache baada ya Evra kucheza chini kiwango dhidi ya Iceland. Kiungo mkabaji Yann M'Vila pia ana majeruhi ya enka ambayo yatamfanya asicheze mchezo wa kwanza na Alou Diarra anategemewa kumbadili.
Lakini hiki ni kikosi tofauti sana na kile kilichoenda kwenye kombe la dunia 2010 chini Raymond Domenech nchini South Africa. Golikipa Hugo Lloris sasa ni nahodha, lakini Phillipe Mexes, M'Vila na Karim Benzema ambaye yupo kwenye form sasa hivi, wote waliikosa michuano ya WOZA 2010 hivyo hawakuwemo kwenye aibu iliyopita. Lakini hili haliwezi kusemwa linapojitokeza jina la Frank Ribery, ambaye kwa sasa yupo desparate kuweza kurudisa imani na upendo wa wafaransa. Baada ya miaka 3 bila kufunga bao, Ribery alifunga mara mbili katika mechi 2 za kirafiki zilizopita. Ikiwa ataanza japo kuileta nusu ya uwezo anaonyesha Bayern Munich akiwa kwenye jezi za Blue, then Les Bleus wanaweza kuwashangaza wengi.
WACHEZAJI MUHIMU
Karim Benzema
Tumaini kubwa la soka la Ufaransa lilikuwa na mwanzo mmbaya kwenye career yake ndani ya timu ya taifa ya Ufaransa kwenye michuano ya Euro 2008, pale alipotuhumiwa kwa pamaja na Samir Nasri kwa kutokuwa na heshima kwa wachezaji wakubwa na kwa kutompasia mipra mingi Thierry Henry. Akaachwa kwenye kombe la dunia 2010, lakini amekuwa ndio mfungaji bora wa Ufaransa chini ya Blanc, akifunga mabao matano katika mechi 17, likiwemo goli la ushindi dhidi ya Brazil. Huku akiwa amemaliza msimu wa mafanikio na Real Madrid akifunga mabao 32, huku akitamba kwamba amekuwa mchezaji mzuri zaidichini Jose Mourinho. Na kama hayo maneno yataonekana kwenye vitendo basii Ufaransa itaifadika sana.
Samir Nasri
Mpaka aliposhinda kombe la premier league na Manchester City mwezi uliopita, Nasri alikuwa ameshinda kombe moja tu kwenye maisha yake ya soka la kulipwa: alipofunga goli la ushindi kwenye fainali ya Euro 2004 kwa timu ya vijana wa miaka 17. Nasri ni moja ya sehemu ya kundi 'Kizai cha 87' kinachowahusisha wachezaji waliozaliwa mwaka 1987 na kwa sasa wakiwa ndio wanaelekea kwenye vilele vya viwango vyao wakiwa kwenye timu ya taifa ya wakubwa. Kundi hilo lilikuwa linawahusisha Benzema, Hatem Ben Arfa, Jelemu Menez na Blaise Matuidi - wote walicheza kwenye Euro 2004, na sasa wapo kwenye Euro 2012 ya wakubwa. Kama kiungo mchezeshaji Nasri anayo nafasi ya kuifanya timu ikacheza soka zuri la kushambulia na ahatimaye kuiletea timu ushindi. Ni jukumu ambalo amekuwa alilitumikia siku nyingi, sasa hivi anayo nafasi ya kuonyesha kama kweli anastahili.
Yann M'Vila
Kiungo mkabaji anatarajiwa kuuzwa kwa mapesa mengi mara baada ya michuano hii, na klabu yake. Rennes, inaweza ikataka kuongeza beikama atacheza vizuri kwenye Euro.M'Vila alikuwa na bahati kuikosa world cup, alitoswa na Domenech lakinii chini ya Blanc amejihakikishia nafasi ya kudumu. Akiwa na miaka 21, amekuja kuwa mchezaji muhimu wa Ufaransana kwa jinsi inavyocheza, kuvunja mashambulizi ya wapinzani na kushambulia kutokea kwenye kiungo huku akiwa na uwezo mkubwa wa kupiga pasi. Ameshajulikana kwamba ataikosa mechi yake ya kwanza ya Euro dhidi ya England na anategemewa kurudi dimbani kwenye mechi ya Ukraine.

Subscribe to:
Posts (Atom)