NSAJIGWA: MKATABA WANGU UMEISHA YANGA, NA SINA MPANGO WA KUOMBA MKATABA MPYANSAJIGWA: MKATABA WANGU UMEISHA YANGA, NA SINA MPANGO WA KUOMBA MKATABA MPYA
Aliyekuwa
nahodha wa Taifa Stars Shedrack Nsajigwa ambaye msimu uliopita alikuwa
akiichezea klabu ya Yanga amesema haitatokea hata siku moja akaomba
mkataba mpya Yanga kwa sababu anajiamini yeye ni mchezaji mzuri.
Amesema “Mimi mkataba wangu na Yanga umeshaisha kwa hiyo mimi ni
mchezaji huru, nilijua siwezi kuwepo Yanga milele, mkataba umeisha
naangalia mambo mengine kwa sababu nilisaini mkataba wa miaka miwili
nikijua siku moja nitaondoka.”
Kuhusu yeye kuomba mkataba mwingine baada ya aliokua nao kumalizika,
Nsajigwa amesema, “Mie ni mchezaji bwana najiamini na kazi yangu, siwezi
kuomba mkataba bado nguvu ya kufanya kazi ninayo siwezi eti kuomba
mkataba na timu fulani, aaah never…. sijawahi na haitatokea”
Inaaminika kwamba Nsajigwa ametemwa Yanga kwa sababu alikuwa kiongozi wa
wachezaji wenzake kugoma kwa kudai malipo yao, stori nyingine ambazo
hazijathibitishwa ni kwamba Club hiyo ina mpango wa kuwaondoa wachezaji
wote wenye umri mkubwa na kutaka damu changa kwa ajili ya msimu ujao.
No comments:
Post a Comment