KIINGILIO MECHI YA TAIFA STARS, GAMBIA 3,000/-
Kiingilio
cha chini ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa
Stars) na Gambia (The Scorpions) itakayochezwa Jumapili (Juni 10 mwaka
huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 3,000.
Watazamaji
watakaolipa kiingilio hicho ni watakaokaa kwenye viti vya rangi ya bluu
na kijani ambavyo ni 36,693 kati ya jumla ya viti 57,558 vilivyopo
katika uwanja huo wa kisasa. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ni
sh. 5,000.
Kwa
upande wa VIP C watalipa sh. 10,000 wakati VIP B ni sh. 20,000.
Kiingilio kwa jukwaa la VIP A ambalo linachukua watazamaji 748 tu ni sh.
30,000 kwa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni.
Tiketi
zitaanza kuuzwa Jumamosi (Juni 9 mwaka huu) kuanzia saa 2 asubuhi
kwenye vituo vya Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Shule
ya Sekondari Benjamin Mkapa, Soko Kuu la Kariakoo na Uwanja wa Taifa.
Siku ya mechi pia mauzo yatafanyika katika vituo hivyo na baadaye
kuhamia Uwanja wa Taifa.
GAMBIA YATARAJIA KUINGIA LEO DAR ES SALAAM
Timu
ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) inatarajia kuwasili nchini wakati
wowote kuanzia leo (Juni 6 mwaka huu) tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya
Taifa Stars.
Kamati
ya Maridhiano inayoendesha Chama cha Soka Gambia (GFA) hadi leo mchana
ilikuwa haijatuma taarifa rasmi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) juu ya ujio wake.
Lakini
vyombo vya habari vya Gambia vimeripoti kuwa timu hiyo ikiwa na
wachezaji 23 na viongozi tisa ilitarajiwa kuondoka huko leo kuja Dar es
Salaam tayari kwa ajili ya mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na
washabiki wengi nchini.
Kwa
mujibu wa Ofisa Habari wa GFA aliyekaririwa na vyombo vya habari vya
nchi hiyo, Bakary Balder, msafara wa timu hiyo utaongozwa na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Michezo, Malang Jassey. .
Mbali
ya Jassey, viongozi wengine katika msafara huo ni Ofisa Utawala wa timu
Modou Sowe, Kocha Luciano Machini, makocha wasaidizi Peter Bonu Johnson
na Lamin Sambou, Kocha wa makipa Alhagie Marong, mtaalamu wa tiba
mbadala (physiotherapist) Pa Matarr Ndow, Mtunza vifaa Sanna Bojang na
Daktari wa timu Kalifa Manneh.
Wachezaji ni Musa
Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin Basmen Samateh, Ousman
Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba Mal Ceesay, Demba
Savage, Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou Ceesay, Pa Modou Jagne,
Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa, Sulayman
Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na Saloum Faal.
TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA
Tanzania
imepanda kwa nafasi sita kwenye orodha ya viwango ya Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) iliyotolewa leo (Juni 6 mwaka huu) na
shirikisho hilo.
Kwa
viwango vya Mei mwaka huu, Tanzania ambayo timu yake ya Taifa (Taifa
Stars) inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa namba 145 hivi
sasa imefika nafasi ya 139 ikiwa na pointi 214.
Mei
26 mwaka huu Taifa Stars ilicheza mechi ya kirafiki na Malawi na kutoka
suluhu. Malawi yenye pointi 324 imeporomoka kwa nafasi tano kutoka ya
102 hadi 107.
Ivory
Coast ambayo katika mechi yake ya mwisho Juni 2 mwaka huu iliifunga
Taifa Stars mabao 2-0 imeporomoka kwa nafasi moja kutoka ya 15 hadi 16
ikiwa na pointi 943. Hata hivyo ndiyo inayoongoza kwa upande wan chi za
Afrika katika viwango hivyo.
PROGRAMU YA TAIFA STARS KWA MECHI YA GAMBIA
JUMATANO JUNI 6
01.00 asubuhi Mazoezi- Uwanja wa Karume
10.00 jioni Mazoezi- Uwanja wa Taifa
ALHAMISI JUNI 7
10.00 jioni Mazoezi- Uwanja wa Taifa
IJUMAA JUNI 8
10.00 jioni Mazoezi- Uwanja wa Taifa
JUMAMOSI JUNI 9
04.00 asubuhi Mkutano na Waandishi wa Habari- Ukumbi wa TFF
11.00 jioni Mazoezi- Uwanja wa Taifa
No comments:
Post a Comment