MARADONA; MIMI NI MTU NILIYEKUFA KWA DAKIKA NNE,SASA NAJUA
MAISHA NI NINI
Umaarufu wake katika soka ulianzia katika timu ya Argentina Juniors na
taratibu baada ya hapo alizichezea timu za Boca Junior,FC
BarcelonaNapoli,Sevilla na Newll's Boys .Amewahi kutwaa tuzo mbalimbali
katika maisha yake ya soka na mwaka 2000 alipewa tuzo ya mwanasoka bora
wa Karne sambamba na Pele wa Brazili heshima waliyopewa na Fifa.Msomaji
wa number10 unajua namna Diego Maradona alivyoishi maisha yakr ya
utotoni? Vipi kuhusu uwezo wa familia yake? msikilize Diego mwenyewe
katika maala hii ya maswali na majibu.
Swali: Ilikuwaje wakati unajifunza soka?
Maradona;
Unajua nilijifunza soka nyuma ya nyumba yetu,kuikuwa na uwanja
naotumiwa na timu moja ya daraja la nne,niicheza pale kila siku wakati
watoto wengine walipokwenda makwao mimi niliendelea kucheza kwa saa
mbili zaid giza likiwa tayari limeshaingia.Nilikuwa sioni kitu gizani
,nilikuwa napiga tu mpira nilichokuwa nazingatia ni miti miwili
(magoli).Miaka 10 baadae niliposaini mkataba wangu wa kwanza na
Argentina Juniors ndipo nilipobaini uamuzi ule wa kucheza gizani ulikuwa
sahihi.
Swali:
Wewe ulizaliwa Favel Fiorito,eneo linalosifika kwa umasikini katika
jiji la Buenos Aires nini hasa ulichokuwa ukifikiria wakati huo,kwa
sababu hujasahau watu wa kule na bado unaendelea kuwa nao karibu?
Maradona;
Watu masikini hawawezi kamwe kukuahau au kukulaghai,wengi wao ni
marafiki zangu na mmoja wao ni kocha wangu,Coppola,huyu alikuwa
akiniibia fedha zangu,watu wa Fiorito wapo katika hali ya umasikini.Leo
hii kunaweza kuwa na mambo yanayotoa picha ya maendeleo lakini umasikini
bado ni ule ule tangu wakati nikiishi pale,lakini wanasiasa na watu
walio karibu na serikali wameendelea kuwa matajiri zaidi na
zaidi.Niliwahi kuwa na nafasi ya kuwa kama wao lakini nilikataa kwa
sababu ningewaibia masikini,kuna wakati nilizungumza na watu wa
Argentina waliojiingiza katika maisha ya sisa na niliwaambia kila kitu
ambacho hawakutaka kukisikia.
Swali: Katika maisha hayo ya umasikini,unazungumziaje namna baba yako alivyokuwa akiangaikia familia?
Maradona;Nakumbuka
hali ilivyokuwa mara ya baba kurudi kutoka kazini,hakuweza kuwa na
chakula cha kutulisha watoto wote sisi nane.Watu walioshiba hawawezi
kulijua hilo kamwe,hususani wale ambao hawakuwahi kuwa na njaa,dada
yangu alilazimika kula chakula pungufu ili tu chakula kibaki kwa ajili
yangu wakati wa jioni kwa mazingira kama hayo unalazimika kuwa na huruma
na mwenye kujali wasio na chakula.Historia yangu ya utotoni kamwe
siwezi kuisahau hivi hivi,Mama yangu alilazimika kudanganya anaumwa
tumbo ili tu aweze kupata chakula kwa ajili ya watoto wake na wakati
wote alikuwa akiangalia kwenye mabakuli kuhakikisha kama kuna chakula
kwa watu wote.Huo ndiyo umasikini,mama yako analazimika kudanganya,mtu
unaweza kuuita uongo wa kisayansi,lakini hiyo ndiyo hali halisi ya
maisha ilivyokuwa,nakwambia ukweli.
Swali:
Huo ni umasikini kama unavyosema lakini kuna watu wanasahau mapema hali
hiyo,wewe vipi unaendelea kuwa na fikra za maisha ya utotoni?
Maradona;
Nisingeweza kusahau,sisahau umasikini ni wazamani kuliko utajiri,baba
yangu alikuwa akifanya kazi Kvantaca ( eneo la sokoni) na wakati wote
alikuwa akibeba mifuko mizito hata wakati ambao umri wake ulikuwa
mkubwa.Baada ya kurudi nyumbani Mama alikuwa akimuwekea bonge la barafu
shingoni ili kupunguza maumivu na sisi watoto wake wakati huo tulikuwa
pembeni,huo ulikuwa kama utamaduni ambao hauwezi kuondoka katika fikra
zangu
Swali: Tuzungumzie mambo yaliyozoeleka kwa watu masikini nini hasa unachokumbuka zaidi ukiwa mtoto?
Maradona;
Heshima,lakini pia hatukuwa na vitu kama sherehe za kuzaliwa,hatukuwa
na fedha kwa mambo hayo,marafiki familia na binamu walikuwa wakikubusu
na hiyo ilikuwa zawadi kubwa tu.Hali ni tofauti kwa wale ambao ni
matajiri,sina shaka kwamba kuna watu wanaofanya makubaliano na wanasiasa
na wanasiasa wanatumia pale wanapohitaji kufanya mambo hayo.Kama wewe
hukubali katika utaratibu huo unaonekana kichaa,ndiyo mimi kichaa ni
bora niwe kichaa kuliko kukubali nitoe kitu ambacho walitakiwa
kunihudumia mimi.Unajua mimi ni kama mtu aliyekufa kwa dakika nne na
sasa najua maisha ni nini.
Swali:
Kuna walijituma kupunguza umasikini mfano ni mwanamuziki,Bono
amezunguka dunia nzima kuwashawishi marais wa nchi tajiri kupunguza
madeni kwa nchi masikini na ameweza hata kula chakula cha mchana na
aliyekuwa Rais wa Marekani,George W Bush
Maradona;
Najua jambo moja ambalo sitoweza kulifanya kamwe ni kupata ujasiri wa
kula chakula na Bush,sitaona nimefanya jambo jema kwa kula chakula na
muuaji wa halaiki.
Swali: Nini hasa unadhani kifanyike kuleta mabadiliko?
Maradona;
Nini cha kufanya?Ni vigumu kubadili mambo,lakini muhimu tuyazungumze
matatizo kwanza,bahati mbaya Papa (baba mtakatifu) hataki kuzungumzia
matatizo na hata anapofanya hivyo anachofikiria ni kitu kimoja,namna ya
kuitunza Vatican kama ilivyo kwa Wamarekani.Vatican ni tajiri sana,dola
yao ina ngvu.Papa John Paul II hakuwahi kulifahamu kwa undani kuhusu
Afrka,hakwenda pale kubusu ardhi na kuwapa chakula watoto masikini na
pia hakuwahi kuijua Argentina.Lakin i ni yeye anayechukua dola million
150 inayotokana na matangazo ya kondomu,asasi inatoa fedha hizo kwa
ajili ya kampeni ya matangazo ya biahara,lakini yeye Papa hakuwahi kujua
lolote kuhusu kondomu,alikuwa anachukua tu fedha.Leo hii hakuna
anayezungumza namna Papa alivyoitupa Afrika na watu masikini
wameongezeka tangu kuangushwa kwa ukuta wa Berlin.
Swali: Wewe ni rafiki mkubwa wa rais wab Cuba Fidel Castro,mmekutana vipi na mtu huyu?
Maradona;
Mwaka 1987 nilipewa tuzo mbili moja na Cuba nyingine na
Marekani,niliwaambia Wamarekani wakae na tuzo yao na moja kwa moja
nikaenda Cuba.Nilikutana na Fidel na tukazungumza kwa saa tano kuhusu
Che Guevara (mwanamapinduzi wa zamani wa Argentina) .Nikweli nilisoma
siku nyingi habar za mapinduzi,busara za Che na Fidel na nikajikuta
navutiwa na Fidel na kwa mtazamo wangu yeye ni sawa na Simba
anayepigania eneo lake,ni mwanasiasa pekee ambaye hana mtazamo wa
kuwaibia masikini.
Swali: Umewaji kusema vita kubwa uliyowahi kupamana nayo ni kuachana na matumizi ya madawa?
Maradona;
Ndiyo,ni vita kubwa,lakini ilibidi nipambane nayo kwa bidii na
niliamini kuwa ilikuwa vita ngumu,ni kama uko katika mechi ambayo
umeshindwa na unataka kushinda kwa namna yoyote ile lakini hakuna msaada
wa kupata ushindi nje ya kutimiza majukumu yako.
Swali:
Wakati ukichezea Napoli mwaka 1991 ulifungiwa kwa kosa la kutumia dawa
za kuongeza nguvu,lakini baadaye ulisema kwamba kufungiwa kwako ni
kulipiza kisasi baada ya Argentina kuitoa Italia katika kombe la Dunia
mwaka 1990.
Maradona; Naamini hivyo,naamini wale Mafia walikuwa na fedha nyingi sana na walikuwa na hasira na mimi.
Swali: Ilikuwaje hadi ukafungiwa kucheza soka?
Maradona;
Walikuta Cocaine kidogo na kunifungia kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja
kucheza soka.Hiyo yote naamini ilikuwa sababu ya kunitoa nje ya soka kwa
maisha yangu ya soka,walidhani wagenimaliza na kuniacha nimekufa
mtaani.
Swali: Uliwaambia nini wachezaji wenzako kabla ya mechi yako ya mwisho ukiwa kama mchezaji mwaka 1997,nasikia wengi walilia!!
Maradona;
Ndiyo,wote tulilia nilizungumza na mchezaji mmoja mmoja niliwaaga
katika soka na nilifahamu kwamba sitovaa tena jezi nikiwa mchezaji.

No comments:
Post a Comment