Tuesday, June 12, 2012

WAREMBO 12 wanaotarajia kuwania taji la kitongoji cha Kigamboni mwaka huu

WAREMBO 12 wanaotarajia kuwania taji la kitongoji cha Kigamboni mwaka huu 'Miss Kigamboni City 2012' leo Jumatano wanatarajiwa kufanyiwa usaili kwa ajili ya kuanza safari ya kumpata mshindi wa shindano hilo litakalofanyika Ijumaa kwenye ukumbi wa Navy Beach jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa shindano hilo, kutoka kampuni ya K&L Media Solutions, Somoe Ng'itu, alisema jana kuwa maandalizi ya zoezi hilo yamekamilika na wanachosubiri ni siku ya shindano ifike.
Alisema kuwa kitongoji hicho kina warembo wenye sifa na wanaojiamini ambao wamepania kurudisha taji la Miss Tanzania kwenye Kanda ya Temeke.
Aliongeza kuwa ili kuboresha shindano hilo bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia maarufu Wazee wa Ngwasuma na msanii na mchekeshaji mahiri hapa nchini, Mpoki watatumbuiza kwenye kinyang'anyiro hicho.
"Tunawaomba wadau wa sanaa ya urembo kufika kushuhudia mrembo wa Kigamboni atakavyopatikana, ni Kitongoji kilichoko sehemu pekee hapa nchini na kulikosa kushuhudia itakuwa ni kujinyima burudani wewe mwenyewe," alisema mratibu huyo.
Aliwataja warembo watakaochuana kuwa ni pamoja na Susanne Jeremiah, Agness Goodluck, Elizabeth Boniface, Dorothea Kessy, Esther Albert, Edda Silyvester, Sophia Martin, Doreen Kweka, Khadija Kombo, Linnah David, Rosemary Peter na Winnie Karaya.
Aliwashukuru wadhamini ambao wamejitokeza kusaidia shindano hilo ambao ni Redd's, Dodoma Wine, hoteli ya Hope Country, Screen Masters, Global Publishers, Nobro Collections, Times FM na Clouds FM.
Aliongeza kuwa warembo watakaoshika nafasi tatu za juu kutoka katika shindano hilo wataungana na wenzao kutoka vitongoji vya Kurasini na Chang'ombe ili kuwania taji la Kanda ya Temeke baadaye mwaka huu.

MESSI AWAFUNDISHA SOKA WABRAZIL: APIGA HAT TRICK ARGENTINA WAKIUA BRAZIL 4-3

MESSI AWAFUNDISHA SOKA WABRAZIL: APIGA HAT TRICK ARGENTINA WAKIUA BRAZIL 4-3

 

 

Thursday, June 7, 2012

WENDAWAZIMU WANAONGOZA KWA USHAMBULIAJI LIGI YA ITALY

Maneno ya Cesare Prandelli alipomrithi Marcello Lippi kama kocha wa timu ya taifa baada ya kombe la dunia mwaka 2010 ni kwamba ataifanya Azzuri ivutiwa kwa kucheza soka zuri la kushambulia. Kwa hakika amejitahidi sana huku akitambulisha utaratibu wa 'ethical code' (wachezaji wanaokuwa wamesimamishwa kwa makosa ya kinidhamu hawatoitwa timu ya taifa) na kusisitiza katika kuwapa nafasi zaidi viungo wenye ufundi zaidi katika timu yake. Wazo ni kuifanya Italia kucheza kwa staili yake ya mfumo wa tiki-taka, staili inayopendelewa zaidi na Wahispania.

Akiuacha mfumo wa siku nyingi wa kujenga ukuta wa chuma na kucheza kwa mashambulizi ya kushtukiza kwa ajili ya mfumo ambao unatumia na Spain, ambao mpaka sasa umeleta matokeo ya mchanganyiko. italy haikufungwa hata mechi moja kwenye hatua ya kufuzu, lakini wamekuwa wakifungwa kwenye mechi za kirafiki. Skendo ya upangaji wa matokeo ambayo inaliandama soka la nchi hiyo kwa miaka mingi sasa, haitegemewi kuwa na madhara makubwa sasa hivi kuliko ilivyokuwa katika miaka 1982 na 2006, sababu kubwa ni kwa kuwa ni wachezaji wachache wa kikosi cha sasa wameguswa na kashfa hiyo, lakini suala hilo bado linabakia kuwa sio zuri kwa wachezaji.

Droo ya group C haikuwa nzuri kwa Italy, lakini atleast mechi yao dhidi ya Spain itakuwa ya kwanza. Na kupata pointi kutoka kwenye mechi hiyo ni jambo ambalo linawezekana, kwa kuangalia Spain huwa na kawaida ya kuanza vibaya michuano mikubwa, ukiangalia kombe la dunia lilopita walipofungwa na Uswis katika mechi ya kwanza makundi. Baada ya mechi hiyo atleast kidogo mambo yanaweza kuwa mazuri dhidi ya Croatia na Ireland.

WACHEZAJI MUHIMU

Gianluigi Buffon
Nahodha amerudi kwenye kiwango chake baada ya majeruhi yaliyomkumba msimu wa  2010-11. Ukifikiria namna safu ya ulinzi ilivyokuwa dhaifu, Azzuri wanahitaji kuwa na Buffon mwenye kiwango cha juu ili kuepeuka balaa. Ni uchizi sasa kufikiri kwamba safu ya ulinzi ambayo siku zote imekuwa ndio nguzo ya timu ya taifa ya Italia, sasa hivi ndio ulipo udhaifu wao, lakini hapa ndipo tulipo, na sasa tumaini lote lipo kwa Buffon na mikono pamoja na miguu yake kutatua hilo tatizo.


Mario Balotelli
Mario Balotelli alisema hatoshangilia goli mpaka atakapofunga goli la ushindi kwenye world cup au Euro, hivyo hii ndio nafasi pekee kumuona Super Mario akicheza kwa furaha baada ya kutupia kambani. Tuache utani, huu ni muda wake kuweza kuonyesha kwanini makocha wamuamini na kumpa nafasi. Balotelli ana nguvu, ujuzi na kimo kizuri, Anachohitaji ni kutulia na kutumia vizuri nafasi atakazopata huku akijiepusha na suala la nidhamu mbovu. Akifanikiwa kwenye hayo atatisha.


Daniele De Rossi
Katika kiungo ambacho kimejaa wapiga pasi mafundi zaidi, De Rossi ndio kiumbe anayetegemewa kusambaza minguvu yake. Shujaa huyu wa Roma ndio sasa anaelekea kwenye kilele chake, akiwa ameshaji-commit kwenye klabu yake, sasa yupo huru kufikiria timu ya taifa tu. Atakuwa na shughuli ngumu katika kupambana na kuizuia safu ya ulizni wa timu ambayo ni dhaifu kutoguswa

 JE SAFU YA USHAMBULIAJI YA MACHIZI ITAFANYA VIZURI?
Mara tu Giueseppe Rossi alipoumia, mikono ya Prandelli ilikuwa imefungwa. Akawa hana chaguo lingine zaidi ya kuwatumia Balotelli na Antonio Cassano. Hii haihusu suala la uwezo  - -wachezaji wote wawili wana vipaji vikubwa tataizo ni nidhamu: wote wawili wana matukio mengi ambayo yanahusu ukosefu wa nidhamu na tabia nyingine tofauti,ndani na nje ya uwanja. Hivyo hilo ni tatizo ambalo Prandelli inabidi alitafutie suluhisho.

YANGA NA SIMBA MAMA YAO NI MMOJA




Kikubwa zaidi ninachojaribu kukiangalia ni jinsi ambavyo viongozi wa vilabu vya SIMBA na YANGA wasivyopenda kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa, mwenyekiti wa SIMBA ameongelea kwa jazba kubwa sakata la beki wa timu yake Kelvin Yondani kusajiliwa na Yanga, si ajabu kesho tu tukasikia viongozi wa YANGA nao wakilijibu hili kwa mbwembwe.
 

Lakini mwisho wa siku ni lazima tukubali kuwa viongozi wote hawa wa simba na yanga wana mapungufu makubwa sana katika utendaji wao wa Kazi, na namna wanavyoendesha vilabu vyao na mpira wa Tanzania kwa ujumla.

Viongozi hawa wa SIMBA na YANGA Wamekuwa wakifanya mambo mengi sana ya ajabu ajabu. SIMBA na YANGA ni vilabu ambavyo vinatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na vilabu vingine vidogo hapa nchini.
Lakini kwa mambo ambayo yamekuwa yakifanyika ndani ya vilabu hivi vikubwa ni ya ajabu sana na ya kusikitisha mno.

Kwa sakata hili la KELVIN YONDANI kumekuwepo na watu ambao wamekuwa wakijaribu kumshutumu mchezaji huyo, lakini mimi binafsi siwezi kumshutumu hata kidogo kwanza, hatujui wakati anasainishwa mkataba na Yanga alikuwa katika mazingira gani labda alitekwa na kulazimishwa,

Pili, labda aliamua tu kusajili huku akisema liwalo na liwe hao Simba wenyewe wamenisainisha mkataba kwa 'mkopo' wakati Yanga wamekuja mezani na mipesa yote hii.
Tatu, kusukumwa na hisia za kukumbuka manyanyaso yasiyoisha ya kushutumiwa kufungisha, mara ugomvi na baadhi ya viongozi Simba.Nne, kutokutambua umuhimu na kuuheshimu mkataba wake na Simba.
Kwa nchi za wenzetu zilizoendelea kitendo cha mchezaji kusaini mkataba ni kitu muhimu mno, lakini huku kwetu umuhimu na thamani ya mkataba hujulikana wakati wa matatizo hasa pale tu mchezaji anapotaka kuondoka na kwenda kujiunga na klabu nyingine.

Mimi nina uhakika wa zaidi ya asilimia mia moja kwamba hakuna mchezaji anayechukua mkataba na kuusoma, kuuelewa vipengele vilivyomo kabla ya kuusaini.


Ninachojua ni kwamba mchezaji huwa anaangalia napata kiasi gani…nazungumza hili kwasababu nina uhakika nalo na lilishawahi kunitokea wakati nacheza mpira, wakishakubaliana anaonyeshwa pakuweka saini na dole gumba kisha anachukua mzigo wake na kusepa.

Ndio maana wenzetu huwa wanawatanguliza wawakilishi, mchezaji anapokwenda kusaini mkataba ni lazima kuwa na meneja/wakala ama mwanasheria wake, lakini hapa kwetu Tanzania ni kinyume kabisa,wachezaji wenyewe hata darasa la saba hawajamaliza halafu anaenda kusaini mkataba tena wa kisheria tena ulioandikwa kwa lugha ya kiingereza, je ana uwezo wa kuelewa? au tunadanganyana tu na kupotezeana muda.

Professionalism inatakiwa kuanzia kwa viongozi wa vilabu kabla ya wachezaji, kwa maana viongozi wanatakiwa kusimamia sheria kama zilivyo, lakini cha kustaajabisha viongozi hao hao wa vilabu ndio wanakuwa vinara kwa kupindisha sheria hizo na kushindwa kwenda nazo sambamba.

Hivyo inapotokea ishu kama hii ya leo pasipo kufuata uweledi ndipo mmoja anaonekana kuonewa au kwenda against na mwenzake lakini kumbe wote wana makosa makubwa.


Ina maana hawa viongozi wanaowasainisha hiyo mikataba ya kisheria hao wachezaji hawajui kama hawana elimu ya kutosha ya kuisoma na kuielewa hiyo mikataba jamani hii lugha ya kiingereza inayotumika kwenye hii mikataba (mimi mwenyewe inaniacha ) ni mchezaji gani wa kitanzania mwenye uwezo wa kuisoma na kuielewa kabla ya kusaini na kuweka dole gumba? kama kweli hawa viongozi wanawatakia mema hawa wachezaji kwanini hiyo mikataba isiwekwe kwenye lugha ya Kiswahili angalau wanaweza kuambulia kitu. ( au kisheria ni lazima mkataba uwe kwenye lugha ya kiingereza ?)
Ishu kama hii ya YONDANI bila kuhangaika sana ebu tuangalie KANUNI ZA USAJILI zinasemaje


Kanuni ya 57
Uhamisho wa mchezaji

(1) Kilabu inaweza kumhamisha mchezaji kutoka kilabu kimoja hadi kingine, kwa madhumuni ya kumsajili, baada ya ligi kumalizika, au katika kipindi cha usajili wa katikati ya msimu. Kilabu inayotaka kumsajili mchezaji aliyesajiliwa na kilabu kingine au mwenye mkataba na kilabu kingine, italazimika kuafikiana na kilabu yake kabla ya kumsajili mchezaji huyo. Hata hivyo kilabu ambayo itaruhusiwa kusajili mchezaji katikati ya msimu ni ile ambayo haijatimiza wachezaji thelathini (30) au ile ambayo imempa mchezaji wake ITC ya kwenda kucheza soka nje ya nchi, au ile ambayo mchezaji wake amehamia kilabu kingine cha ndani kwa mujibu wa kanuni hii.

Kanuni ya 45
Usajili na uhamisho wa wachezaji

(4) Mchezaji ana uhuru wa kujisajili na kilabu kingine katika msimu mmoja iwapo kutakuwa na maelewano kati ya kilabu yake na ile inayotaka kumsajili.
(5) Kilabu inawajibika kuingia mkataba na mchezaji wa kuichezea lakini mkataba huo ni lazima uthibitishwe na TFF. Ada ya kuthibitisha mkataba ni shilingi elfu hamsini (50,000/=).

(6) Mchezaji ambaye ameingia mkataba wa zaidi ya msimu mmoja hatoruhusiwa kujisajili na kilabu kingine kabla ya kilabu yake mpya kuafikiana na kilabu yake ya zamani.

Kanuni ya 56
Katazo

Haitaruhusiwa kwa mchezaji yeyote kutia saini kwenye mikataba wa vilabu viwili tofauti kwa wakati mmoja na inayohusu kipindi kimoja. Mchezaji atakayesaini mikataba ya timu mbili tofauti kwa wakati mmoja, ataadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 44 (4) ya kanuni hizi.
Kutokana na vipengele hivyo hapo juu hakuna mchezaji ambaye anaweza kuhama timu moja kwenda timu nyingine kihuni huni tu pasipo kufuata kanuni na taratibu.

Sakata la Simba na Azam juu ya usajili wa Ibrahim Jeba.
Lazima tusiwe wanafiki, waswalihi wanasema mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu mchungu, wakati tukiwa tunalijadili sakata hili la Yondani si vibaya pia tukaliwe mezani sakata linalomuhusu mchezaji Ibrahim Jeba aliyesajiliwa na Simba Kutoka Azam pasipo taratibu kufuatwa.


Kanuni ya 44
Masharti ya mikataba kati ya wachezaji na kilabu
(1) Muda wa chini wa mkataba utakuwa kuanzia tarehe ya kuanza kutumika hadi mwisho wa msimu. Muda wa juu wa mkataba utakuwa ni kipindi cha miaka mitano (5). Mikataba ya muda mwingine wowote itakubaliwa kama inafuata Sheria ya Mikataba inavyosema. Mchezaji chini ya umri wa miaka 18 haruhusiwi kuingia kwenye mkataba wa mchezaji wa kulipwa kwa kipindi kinachozidi miaka mitatu (3), sharti lolote linalotaja kipindi kirefu zaidi halitatambuliwa.

(2) Kilabu inayotarajia kuingia mkataba na mchezaji wa kulipwa haina budi kuiarifu kilabu yake ya sasa kwa maandishi kabla ya kufanya makubaliano na mchezaji huyo wa kulipwa. Mchezaji wa kulipwa atakuwa huru tu kuingia mkataba na kilabu nyingine iwapo mkataba wake na kilabu yake ya sasa umekwisha au utakwisha baada ya miezi sita (6). Uvunjaji wowote wa sharti hili utastahili vikwazo vinavyofaa.

Niliposema viongozi wote hasa wa vilabu vya SIMBA na YANGA ndo wenye matatizo makubwa nilikua namaanisha vitendo kama hivi.
Kufanya mazungumzo ya siri na mchezaji pasipo kupata ruhusa ya klabu yake ni kosa kubwa ambalo hata FIFA wanalipiga vita. 

Ina maana Kulwa na Doto hawazijui hizi taratibu na kanuni za kusajili mchezaji ?

Wednesday, June 6, 2012

YANGA YATANGAZA KUMSAJILI KEVIN YONDAN HUKU SIMBA IKIMUONGEZEA MKATABA KELVIN YONDANI.

Leo hii klabu ya Yanga imetangaza kumsajili kinda raia wa Tanzania Kevin Patrick Yondan mwenye umri wa miaka 17,Yondan ambaye anacheza nafasi ya beki wa kati hajajulikana ametokea Klabu gani alizaliwa 9/10/1994.Mkataba wa Yanga na kinda huyo ni wa miaka miwili na unataraji kumalizika msimu wa 2013/2014.


hapa chini ni sehemu ya mkataba wa beki huyo na klabu ya Yanga yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani.
 Mchezaji Kelvin Yondani akisaini mkataba wa usajili mbele ya kiongozi wa Yanga Seif Ahmed usiku huu, katika picha hii Yondani anaonekana akiwa amevaa fulana na timu ya taifa ambazo zimeanza kutumika mwezi mmoja uliopita baada ya stars kuingia mkataba na TBL KUPITIAKilimanjaro.
Taarifa nilizozipata hivi punde Yondani amefuatwa kwenye kambi ya timu ya Taifa iliyopo kwenye Hotel ya Tansoma jijini Dar Es Salaam.

Wakati huo huo Simba Sc imetangaza kumuongezea mkataba wa miaka miwili beki wake wa kati Kelvin Patrick Yondani, mkataba huo mpya ulisainiwa tangia mnamo 23/12/2011 ikiwa ni maboresho ya mkataba wa awali uliokua unafika kikomo mwishoni mwa mwezi uliopita yaani 31/05/2012. Yondani mwenye umri wa miaka 27 pia ni beki wa kimataifa wa Tanzania.


Kelvin Patrick Yondani

First name:Kelvin Patrick
Last name:Yondani
Nationality:Tanzania
Date of birth:10 October 1984
Age:27
Place of birth:

 Baadhi ya michezo ambayo Kelvin Patrick Yondani ameichezea timu ya Taifa ya Tanzania.

TareheNyumbanimatokeo Ugenini

2012-06-02Côte d'Ivoire
2 - 0
Tanzania

2012-05-26Tanzania
0 - 0
Malawi

2012-02-23Tanzania
0 - 0
Congo DR

2011-11-15Tanzania
0 - 1
Chad

2011-11-11Chad
1 - 2
Tanzania

2010-06-07Tanzania
1 - 5
Brazil

2010-01-04Tanzania
0 - 1
Côte d'Ivoire


WEKUNDU WA MSIMBAZI:

SIMBA YAKAMILISHA USAJILI WA SALUM KINJE WA AFC LEOPARDS:

 Taarifa rasmi za uhakika kutoka ndani ya uongozi na kamati ya ufundi ya klabu ya Simba ni kwamba timu hiyo imefanikiwa kukamilisha usajili wa mchezaji bora wa nafasi ya kiungo kwenye ligi kuu ya soka nchini Kenya, Salum Kinje ambaye anaichezea AFC Leopards.

 Kinje ambaye ni mtanzania amesajiliwa na Simba kwa kiasi cha fedha ambacho hakijawekwa wazi na pande zote mbili, lakini amesaini mkataba wa kuitumikia Simba kwa miaka 2 na siku chache zijazo ataanza mazoezi na timu yake mpya inayojiandaa kushiriki michuano ya Kagame Cup inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

UFARANSA:

 Laurent Blanc anaichukua Ufaransa kwenda nayo kwenye Euro 2012 huku akiiongoza timu hiyo kutofungwa katika michezo 20, ambayo inahusisha ushindi dhidi ya Ujerumani, England na Brazil. Lakini kocha huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa bado haipi nafasi kubwa timu. Ufaransa haijashinda mechi yoyote ya mwisho ya michuano mikubwa yenyewe tangu mechi ya nusu fainali ya World Cup 2006 (haikushinda mechi yoyote kwenye Euro 2008 na WOZA 2010), huku wakishika nafasi ya 16, nafasi tisa nyuma ya wapinzani wao England wanaoshika nafasi ya saba kwenye ubora wa viwango wa FIFA.

Blanc bado na maumivu ya kichwa kuhusu upangaji wa kikosi hasa kwenye nafasi ya beki wa kushoto, ambapo Gael Clichy ameonyesha kiwango kizuri kwenye mchi dhidi ya Serbia siku chache baada ya Evra kucheza chini kiwango dhidi ya Iceland. Kiungo mkabaji Yann M'Vila pia ana majeruhi ya enka ambayo yatamfanya asicheze mchezo wa kwanza na Alou Diarra anategemewa kumbadili.

Lakini hiki ni kikosi tofauti sana na kile kilichoenda kwenye kombe la dunia 2010 chini Raymond Domenech nchini South Africa. Golikipa Hugo Lloris sasa ni nahodha, lakini Phillipe Mexes, M'Vila na Karim Benzema ambaye yupo kwenye form sasa hivi, wote waliikosa michuano ya WOZA 2010 hivyo hawakuwemo kwenye aibu iliyopita. Lakini hili haliwezi kusemwa linapojitokeza jina la Frank Ribery, ambaye kwa sasa yupo desparate kuweza kurudisa imani na upendo wa wafaransa. Baada ya miaka 3 bila kufunga bao, Ribery alifunga mara mbili katika mechi 2 za kirafiki zilizopita. Ikiwa ataanza japo kuileta nusu ya uwezo anaonyesha Bayern Munich akiwa kwenye jezi za Blue, then Les Bleus wanaweza kuwashangaza wengi.

WACHEZAJI MUHIMU

Karim Benzema
Tumaini kubwa la soka la Ufaransa lilikuwa na mwanzo mmbaya kwenye career yake ndani ya timu ya taifa ya Ufaransa kwenye michuano ya Euro 2008, pale alipotuhumiwa kwa pamaja na Samir Nasri kwa kutokuwa na heshima kwa wachezaji wakubwa na kwa kutompasia mipra mingi Thierry Henry. Akaachwa kwenye kombe la dunia 2010, lakini amekuwa ndio mfungaji bora wa Ufaransa chini ya Blanc, akifunga mabao matano katika mechi 17, likiwemo goli la ushindi dhidi ya Brazil. Huku akiwa amemaliza msimu wa mafanikio na Real Madrid akifunga mabao 32, huku akitamba kwamba amekuwa mchezaji mzuri zaidichini Jose Mourinho. Na kama hayo maneno yataonekana kwenye vitendo basii Ufaransa itaifadika sana.


Samir Nasri
Mpaka aliposhinda kombe la premier league na Manchester City mwezi uliopita, Nasri alikuwa ameshinda kombe moja tu kwenye maisha yake ya soka la kulipwa: alipofunga goli la ushindi kwenye fainali ya Euro 2004 kwa timu ya vijana wa miaka 17. Nasri ni moja ya sehemu ya kundi 'Kizai cha 87' kinachowahusisha wachezaji waliozaliwa mwaka 1987 na kwa sasa wakiwa ndio wanaelekea kwenye vilele vya viwango vyao wakiwa kwenye timu ya taifa ya wakubwa. Kundi hilo lilikuwa linawahusisha Benzema, Hatem Ben Arfa, Jelemu Menez na Blaise Matuidi - wote walicheza kwenye Euro 2004, na sasa wapo kwenye Euro 2012 ya wakubwa. Kama kiungo mchezeshaji Nasri anayo nafasi ya kuifanya timu ikacheza soka zuri la kushambulia na ahatimaye kuiletea timu ushindi. Ni jukumu ambalo amekuwa alilitumikia siku nyingi, sasa hivi anayo nafasi ya kuonyesha kama kweli anastahili.

Yann M'Vila
Kiungo mkabaji anatarajiwa kuuzwa kwa mapesa mengi mara baada ya michuano hii, na klabu yake. Rennes, inaweza ikataka kuongeza beikama atacheza vizuri kwenye Euro.M'Vila alikuwa na bahati kuikosa world cup, alitoswa na Domenech lakinii chini ya Blanc amejihakikishia nafasi ya kudumu. Akiwa na miaka 21, amekuja kuwa mchezaji muhimu wa Ufaransana kwa jinsi inavyocheza, kuvunja mashambulizi ya wapinzani na kushambulia kutokea kwenye kiungo huku akiwa na uwezo mkubwa wa kupiga pasi. Ameshajulikana kwamba ataikosa mechi yake ya kwanza ya Euro dhidi ya England na anategemewa kurudi dimbani kwenye mechi ya Ukraine.

EXCLUSIVE:FROM JANGWANI

IDDI KIPINGU KUPAMBANA NA MANJI KUWANIA UENYEKITI YANGA

Taarifa zisizo rasmi na za kutoka ndani kabisa ya kamati ya uchaguzi wa Yanga, zinasema  aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la michezo nchini (BMT) Kanali Iddi Kipingu anatarajia kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti wa klabu ya Yanga muda wowote kutoka sasa.


Kipingu ambaye ni mdau mkubwa michezo nchini, akiwa ni mmoja ya watu waliochangia upatikanaji wa vipaji vya wachezaji wengi kama Juma Kaseja, Boniface Pawasa na wengine wengi wakati akiwa mkuu wa wa shule ya Makongo, anatarajiwa kuchukua fomu ndani ya kipindi cha masaa 72 kutoka kutoka sasa.

Kwa maana hiyo sasa Kipingu atakuwa akichuana na mfanyabiashara maarufu ambaye ameshaidhamini Yanga Yusuph Manji ambaye nae tayari ameshachukua fomu rasmi ya kugombea ubosi wa klabu bingwa ya afrika mashariki na kati.

 

MARADONA..

MARADONA; MIMI NI MTU NILIYEKUFA KWA DAKIKA NNE,SASA NAJUA

 

MAISHA  NI NINI
Umaarufu wake katika soka ulianzia katika timu ya Argentina Juniors  na taratibu baada ya hapo alizichezea timu za Boca Junior,FC BarcelonaNapoli,Sevilla na Newll's Boys .Amewahi kutwaa tuzo mbalimbali katika maisha yake ya soka na mwaka 2000 alipewa tuzo ya mwanasoka bora wa Karne sambamba na Pele wa Brazili heshima waliyopewa na Fifa.Msomaji wa number10 unajua namna Diego Maradona alivyoishi maisha yakr ya utotoni? Vipi kuhusu uwezo wa familia yake? msikilize Diego mwenyewe katika maala hii ya maswali na majibu.
Swali: Ilikuwaje wakati unajifunza soka?
Maradona; Unajua nilijifunza soka nyuma ya nyumba yetu,kuikuwa na uwanja naotumiwa na timu moja ya daraja la nne,niicheza pale kila siku wakati watoto wengine walipokwenda makwao mimi niliendelea kucheza kwa saa mbili zaid giza likiwa tayari limeshaingia.Nilikuwa sioni kitu gizani ,nilikuwa napiga tu mpira nilichokuwa nazingatia ni miti miwili (magoli).Miaka 10 baadae niliposaini mkataba wangu wa kwanza na Argentina Juniors ndipo nilipobaini uamuzi ule wa kucheza gizani ulikuwa sahihi.
Swali: Wewe ulizaliwa Favel Fiorito,eneo linalosifika kwa umasikini katika jiji la Buenos Aires nini hasa ulichokuwa ukifikiria wakati huo,kwa sababu hujasahau watu wa kule na bado unaendelea kuwa nao karibu?
Maradona; Watu masikini hawawezi kamwe kukuahau au kukulaghai,wengi wao ni marafiki zangu na mmoja wao ni kocha wangu,Coppola,huyu alikuwa akiniibia fedha zangu,watu wa Fiorito wapo katika hali ya umasikini.Leo hii kunaweza kuwa na mambo yanayotoa picha ya maendeleo lakini umasikini bado ni ule ule tangu wakati nikiishi pale,lakini wanasiasa na watu walio karibu na serikali wameendelea kuwa matajiri zaidi na zaidi.Niliwahi kuwa na nafasi ya kuwa kama wao lakini nilikataa kwa sababu ningewaibia masikini,kuna wakati nilizungumza na watu wa Argentina waliojiingiza katika maisha ya sisa na niliwaambia kila kitu ambacho hawakutaka kukisikia.
Swali: Katika maisha hayo ya umasikini,unazungumziaje namna baba yako alivyokuwa akiangaikia familia?
Maradona;Nakumbuka hali ilivyokuwa mara ya baba kurudi kutoka kazini,hakuweza kuwa na chakula cha kutulisha watoto wote sisi nane.Watu walioshiba hawawezi kulijua hilo kamwe,hususani wale ambao hawakuwahi kuwa na njaa,dada yangu alilazimika kula chakula pungufu ili tu chakula kibaki kwa ajili yangu wakati wa jioni kwa mazingira kama hayo unalazimika kuwa na huruma na mwenye kujali wasio na chakula.Historia yangu ya utotoni kamwe siwezi kuisahau hivi hivi,Mama yangu alilazimika kudanganya anaumwa tumbo ili tu aweze kupata chakula kwa ajili ya watoto wake na wakati wote alikuwa akiangalia kwenye mabakuli kuhakikisha kama kuna chakula kwa watu wote.Huo ndiyo umasikini,mama yako analazimika kudanganya,mtu unaweza kuuita uongo wa kisayansi,lakini hiyo ndiyo hali halisi ya maisha ilivyokuwa,nakwambia ukweli.
Swali: Huo ni umasikini kama unavyosema lakini kuna watu wanasahau mapema hali hiyo,wewe vipi unaendelea kuwa na fikra za maisha ya utotoni?
Maradona; Nisingeweza kusahau,sisahau umasikini ni wazamani kuliko utajiri,baba yangu alikuwa akifanya kazi Kvantaca ( eneo la sokoni) na wakati wote alikuwa akibeba mifuko mizito hata wakati ambao umri wake ulikuwa mkubwa.Baada ya kurudi nyumbani Mama alikuwa akimuwekea bonge la barafu shingoni ili kupunguza maumivu na sisi watoto wake wakati huo tulikuwa pembeni,huo ulikuwa kama utamaduni ambao hauwezi kuondoka katika fikra zangu
Swali: Tuzungumzie mambo yaliyozoeleka kwa watu masikini nini hasa unachokumbuka zaidi ukiwa mtoto?
Maradona; Heshima,lakini pia hatukuwa na vitu kama sherehe za kuzaliwa,hatukuwa na fedha kwa mambo hayo,marafiki familia na binamu walikuwa wakikubusu na hiyo ilikuwa zawadi kubwa tu.Hali ni tofauti kwa wale ambao ni matajiri,sina shaka kwamba kuna watu wanaofanya makubaliano na wanasiasa na wanasiasa wanatumia pale wanapohitaji kufanya mambo hayo.Kama wewe hukubali katika utaratibu huo unaonekana kichaa,ndiyo mimi kichaa ni bora niwe kichaa kuliko kukubali nitoe kitu ambacho walitakiwa kunihudumia mimi.Unajua mimi ni kama mtu aliyekufa kwa dakika nne na sasa najua maisha ni nini.
Swali: Kuna walijituma kupunguza umasikini mfano ni mwanamuziki,Bono amezunguka dunia nzima kuwashawishi marais wa nchi tajiri kupunguza madeni kwa nchi masikini na ameweza hata kula chakula cha mchana na aliyekuwa Rais wa Marekani,George W Bush
Maradona; Najua jambo moja ambalo sitoweza kulifanya kamwe ni kupata ujasiri wa kula chakula na Bush,sitaona nimefanya jambo jema kwa kula chakula na muuaji wa halaiki.
Swali: Nini hasa unadhani kifanyike kuleta mabadiliko?
Maradona; Nini cha kufanya?Ni vigumu kubadili mambo,lakini muhimu tuyazungumze matatizo kwanza,bahati mbaya Papa (baba mtakatifu) hataki kuzungumzia matatizo na hata anapofanya hivyo anachofikiria ni kitu kimoja,namna ya kuitunza Vatican kama ilivyo kwa Wamarekani.Vatican ni tajiri sana,dola yao ina ngvu.Papa John Paul II hakuwahi kulifahamu kwa undani kuhusu Afrka,hakwenda pale kubusu ardhi na kuwapa chakula watoto masikini na pia hakuwahi kuijua Argentina.Lakin i ni yeye anayechukua dola million 150 inayotokana na matangazo ya kondomu,asasi inatoa fedha hizo kwa ajili ya kampeni ya matangazo ya biahara,lakini yeye Papa hakuwahi kujua lolote kuhusu kondomu,alikuwa anachukua tu fedha.Leo hii hakuna anayezungumza namna Papa alivyoitupa Afrika na watu masikini wameongezeka tangu kuangushwa kwa ukuta wa Berlin.
Swali: Wewe ni rafiki mkubwa wa rais wab Cuba Fidel Castro,mmekutana vipi na mtu huyu?
Maradona; Mwaka 1987 nilipewa tuzo mbili moja na Cuba nyingine na Marekani,niliwaambia Wamarekani wakae na tuzo yao na moja kwa moja nikaenda Cuba.Nilikutana na Fidel na tukazungumza kwa saa tano kuhusu Che Guevara (mwanamapinduzi wa zamani wa Argentina) .Nikweli nilisoma siku nyingi habar za mapinduzi,busara za Che na Fidel na nikajikuta navutiwa na Fidel na kwa mtazamo wangu yeye ni sawa na Simba anayepigania eneo lake,ni mwanasiasa pekee ambaye hana mtazamo wa kuwaibia masikini.
Swali: Umewaji kusema vita kubwa uliyowahi kupamana nayo ni kuachana na matumizi ya madawa?
Maradona; Ndiyo,ni vita kubwa,lakini ilibidi nipambane nayo kwa bidii na niliamini kuwa ilikuwa vita ngumu,ni kama uko katika mechi ambayo umeshindwa na unataka kushinda kwa namna yoyote ile lakini hakuna msaada wa kupata ushindi nje ya kutimiza majukumu yako.
Swali: Wakati ukichezea Napoli mwaka 1991 ulifungiwa kwa kosa la kutumia dawa za kuongeza nguvu,lakini baadaye ulisema kwamba kufungiwa kwako ni kulipiza kisasi baada ya Argentina kuitoa Italia katika kombe la Dunia mwaka 1990.
Maradona; Naamini hivyo,naamini wale Mafia walikuwa na fedha nyingi sana na walikuwa na hasira na mimi.
Swali: Ilikuwaje hadi ukafungiwa kucheza soka?
Maradona; Walikuta Cocaine kidogo na kunifungia kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja kucheza soka.Hiyo yote naamini ilikuwa sababu ya kunitoa nje ya soka kwa maisha yangu ya soka,walidhani wagenimaliza na kuniacha nimekufa mtaani.
Swali: Uliwaambia nini wachezaji wenzako kabla ya mechi yako ya mwisho ukiwa kama mchezaji mwaka 1997,nasikia wengi walilia!!
Maradona; Ndiyo,wote tulilia nilizungumza na mchezaji mmoja mmoja niliwaaga katika soka na nilifahamu kwamba sitovaa tena jezi nikiwa mchezaji.

EXCLUSIVE:JANGWANI

ALLY MAYAY ABADILI MAWAZO -ACHUKUA FOMU YA UMAKAMU WA MWENYEKITI

  Mchezaji wa zamani na mmoja ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga ya uongozi uliopita, Ally Mayay amebadili juu ya kutaka kugombea tena ujumbe wa kamati ya utendaji.


Kwaa taarifa nilizonazo kutoka kwake ni kwamba Ally Mayay sasa ameamua kwenda kuchukua fomu za kugombea umakamu uenyekiti wa klabu hiyo aliyoichezea kwa mafanikio miaka kadhaa iliyopita.

TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA

KIINGILIO MECHI YA TAIFA STARS, GAMBIA 3,000/-
Kiingilio cha chini ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Gambia (The Scorpions) itakayochezwa Jumapili (Juni 10 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 3,000.
Watazamaji watakaolipa kiingilio hicho ni watakaokaa kwenye viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo ni 36,693 kati ya jumla ya viti 57,558 vilivyopo katika uwanja huo wa kisasa. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ni sh. 5,000.
Kwa upande wa VIP C watalipa sh. 10,000 wakati VIP B ni sh. 20,000. Kiingilio kwa jukwaa la VIP A ambalo linachukua watazamaji 748 tu ni sh. 30,000 kwa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni.
Tiketi zitaanza kuuzwa Jumamosi (Juni 9 mwaka huu) kuanzia saa 2 asubuhi kwenye vituo vya Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Soko Kuu la Kariakoo na Uwanja wa Taifa. Siku ya mechi pia mauzo yatafanyika katika vituo hivyo na baadaye kuhamia Uwanja wa Taifa.
GAMBIA YATARAJIA KUINGIA LEO DAR ES SALAAM
Timu ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) inatarajia kuwasili nchini wakati wowote kuanzia leo (Juni 6 mwaka huu) tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars.
Kamati ya Maridhiano inayoendesha Chama cha Soka Gambia (GFA) hadi leo mchana ilikuwa haijatuma taarifa rasmi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) juu ya ujio wake.
Lakini vyombo vya habari vya Gambia vimeripoti kuwa timu hiyo ikiwa na wachezaji 23 na viongozi tisa ilitarajiwa kuondoka huko leo kuja Dar es Salaam tayari kwa ajili ya mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na washabiki wengi nchini.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa GFA aliyekaririwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo, Bakary Balder, msafara wa timu hiyo utaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Michezo, Malang Jassey. .
Mbali ya Jassey, viongozi wengine katika msafara huo ni Ofisa Utawala wa timu Modou Sowe, Kocha Luciano Machini, makocha wasaidizi Peter Bonu Johnson na Lamin Sambou, Kocha wa makipa Alhagie Marong, mtaalamu wa tiba mbadala (physiotherapist) Pa Matarr Ndow, Mtunza vifaa Sanna Bojang na Daktari wa timu Kalifa Manneh.
Wachezaji ni Musa Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin Basmen Samateh, Ousman Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba Mal Ceesay, Demba Savage, Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou Ceesay, Pa Modou Jagne, Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa, Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na Saloum Faal.
TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA FIFA
Tanzania imepanda kwa nafasi sita kwenye orodha ya viwango ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) iliyotolewa leo (Juni 6 mwaka huu) na shirikisho hilo.
Kwa viwango vya Mei mwaka huu, Tanzania ambayo timu yake ya Taifa (Taifa Stars) inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilikuwa namba 145 hivi sasa imefika nafasi ya 139 ikiwa na pointi 214.
Mei 26 mwaka huu Taifa Stars ilicheza mechi ya kirafiki na Malawi na kutoka suluhu. Malawi yenye pointi 324 imeporomoka kwa nafasi tano kutoka ya 102 hadi 107.
Ivory Coast ambayo katika mechi yake ya mwisho Juni 2 mwaka huu iliifunga Taifa Stars mabao 2-0 imeporomoka kwa nafasi moja kutoka ya 15 hadi 16 ikiwa na pointi 943. Hata hivyo ndiyo inayoongoza kwa upande wan chi za Afrika katika viwango hivyo.
PROGRAMU YA TAIFA STARS KWA MECHI YA GAMBIA
JUMATANO JUNI 6
01.00 asubuhi  Mazoezi- Uwanja wa Karume
10.00 jioni       Mazoezi- Uwanja wa Taifa
ALHAMISI JUNI 7
10.00 jioni   Mazoezi- Uwanja wa Taifa
IJUMAA JUNI 8
10.00 jioni   Mazoezi- Uwanja wa Taifa
JUMAMOSI JUNI 9
04.00 asubuhi  Mkutano na Waandishi wa Habari- Ukumbi wa TFF
11.00 jioni  Mazoezi- Uwanja wa Taifa

Tuesday, June 5, 2012

EURO 2012:

UZOEFU NI HAZINA MUHIMU: WAJUE WACHEZAJI 12 WALIOCHEZA MECHI NYINGI ZAIDI WALIOPO KWENYE EURO 2012

 Uzoefu mara nyingi ni muhimu sana katika michuano mikubwa na UEFA EURO 2012 kutakuwepo na wachezaji wasiopungua 12 ambao wameshacheza mechi zaidi ya 100 - huku kukiwa kuna wengine wakiwa wanakaribia kufikia idadi hiyo ya mechi.

Wakati kukiwa na mengi ya kuzungumza kuhusu vipaji vya wachezaji wachanga, uzoefu unaweza ukawa na umuhimu katika michuano mikubwa. Wachezaji ambao wameshajifunza vitu vingi  na kukabiliana na presha ya mechi kubwa kwa mara nyingi zaidi wana uthamani mkubwa kwa timu yoyote, na watakuwepo wachezaji namna hiyo wengi wakiuleta uzoefu wao kwenye michuano ya Euro 2012.

Wanaume 12 watasafiri kwenda Poland na Ukraine huku wakiwa na uzoefu wa kucheza mechi zaidi ya 100, in fact, huku Spain's goalkeeper Iker Casillas akiwa anaongoza listi hiyo kwa kucheza mechi 130 akiwa na mabingwa wa ulaya na dunia. Kipa wa Real Madrid alicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Sweden miaka 12 iliyopita na akaweka rekodi mpya Jumatano iliyopita aliposherehekea ushindi wake wa 95 kwenye mechi za kimataifa wakiwafunga 4-1 Korea ya kusini. Akiwa na miaka 31 'Saint Iker' mtakatifu Iker sasa atakuwa kiomba kuisadia Spain kushinda kombe la tatu kubwa mfululizo - huku mchezaji mwenzake Xavi Hernandez ambaye tayari amecheza mechi 108 tangu acheze mchezo wake wa kwanza miaka 12 iliyopita.

Sweden, Jamhuri ya Ireland na Ukraine nazo zimetoa wachezaji waliocheza mechi zaidi ya 100 katika vikosi vyao, Anders Svensson akiwa anamfuatia Casillas kwa kuichezea Sweden mechi 126, akaifuatiwa na mchezaji mwenzie wa timu taifa Olof Melberg akiwa amecheza mechi 113. Shay Given Given wa Ireland akiwa amecheza mechi 121, Robbie Keane amecheza mechi 116, huku wachezaji wawili wa Ukraine Anatoliy Tymoshchuk akicheza mechi 112, na Andrey Shevchenko 107.


Listi ya wachezaji wazoefu zaidi kwenye UEFA EURO 2012:
 

Iker Casillas (Spain, 130 caps)
Anders Svensson (Sweden, 126)
Shay Given (Republic of Ireland, 121)
Giorgos Karagounis (Greece, 117)
Miroslav Klose (Germany, 116)
Robbie Keane (Ireland, 116)
Anatoliy Tymoshchuk (Ukraine, 116)
Dennis Rommedahl (Denmark, 116)
Gianluigi Buffon (Italy, 114)
Olof Mellberg (Sweden, 113)
Xavi Hernández (Spain, 108)
Andriy Shevchenko (Ukraine, 107)
Lukas Podolski (Germany, 97)
Damien Duff (Ireland, 96)
Rafael van der Vaart (Netherlands, 96)
Xabi Alonso (Spain, 95)
Josip Šimunić (Croatia, 95)
Ashley Cole (England, 94)
.

MANCHESTER UNITED OYEEEEE

DONE DEAL: MANCHESTER UNITED YATHIBITISHA KUMSAINI KAGAWA - VIMEBAKI VIPIMO NA KIBALI

 Manchester United wamethibitisha kukamilisha usajili wa mchezaji bora wa ligi kuu ya Ujerumani Shinji Kagawa, aliyekuwa akiichezea Dortmund ambao ndio mabingwa wa Bundesliga.

Kiungo huyo mwenye miaka 23, atajiunga rasmi na United kwa ada ya £12million mwezi ujao baada ya kufaulu vipimo vya afya pamoja na kupata kibali cha kufanya kazi Uingereza.

Taarifa iliyotolewa na United kupitia website yao: "Tuna furaha ya kuwatangazia kwamba tumekubaliana kimsingi na Borrussi Dortmund na Shinji Kagawa kuhamia kwenye klabu yetu.
"Dili litakamilika baada ya mchezaji kufaulu vipimo vya afya na kupata kibali cha kufanya kazi UK.
"Vitu hivi tunategemea vitakamilika ndani ya mwezi ujao."

Mchezaji wa United Rio Ferdinand alifurahishwa sana usajili wa Kagawa na akaandika kwenye ukarasa wake wa Twitter: "Karibu Manchester United Shinji Kagawa. Muda wa kupata mafanikio ni sasa kaka.!"

Monday, June 4, 2012

NSAJIGWA: MKATABA WANGU UMEISHA YANGA, NA SINA MPANGO WA KUOMBA MKATABA MPYANSAJIGWA: MKATABA WANGU UMEISHA YANGA, NA SINA MPANGO WA KUOMBA MKATABA MPYA

NSAJIGWA: MKATABA WANGU UMEISHA YANGA, NA SINA MPANGO WA KUOMBA MKATABA MPYA

 Aliyekuwa nahodha wa Taifa Stars Shedrack Nsajigwa ambaye msimu uliopita alikuwa akiichezea klabu ya Yanga amesema haitatokea hata siku moja akaomba mkataba mpya Yanga kwa sababu anajiamini yeye ni mchezaji mzuri.

Amesema “Mimi mkataba wangu na Yanga umeshaisha kwa hiyo mimi ni mchezaji huru, nilijua siwezi kuwepo Yanga milele, mkataba umeisha naangalia mambo mengine kwa sababu nilisaini mkataba wa miaka miwili nikijua siku moja nitaondoka.”

Kuhusu yeye kuomba mkataba mwingine baada ya aliokua nao kumalizika, Nsajigwa amesema, “Mie ni mchezaji bwana najiamini na kazi yangu, siwezi kuomba mkataba bado nguvu ya kufanya kazi ninayo siwezi eti kuomba mkataba na timu fulani, aaah never…. sijawahi na haitatokea”

Inaaminika kwamba Nsajigwa ametemwa Yanga kwa sababu alikuwa kiongozi wa wachezaji wenzake kugoma kwa kudai malipo yao, stori nyingine ambazo hazijathibitishwa ni kwamba Club hiyo ina mpango wa kuwaondoa wachezaji wote wenye umri mkubwa na kutaka damu changa kwa ajili ya msimu ujao.

BREAKING NEWS: YUSUPH MANJI ACHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA UENYEKITI WA YANGA.


Hayawi hayawi sasa yamekuwa!!!!!
Taarifa rasmi na za uhakika nilizozipata kutoka makao makuu ya klabu ya Dar Young Africans ni kwamba mwanachama maarufu na tajiri wa klabu hiyo, mfanyabiashara Yusuph Mehebob Manji amechukua fomu za kugombea nafasi ya mwenyekiti wa klabu ya Yanga.

Manji ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akiisadia Yanga kiuchumi zaidi, nusu saa iliyopita ameenda kwenye makao makuu ya klabu hiyo na kuchukua fomu za uenyekiti bila kuweka wazi kama kwa ajili yake au amemchukulia mtu kwa ajili kugombea nafasi hiyo.

Kwa siku kadhaa sasa kumekuwa na taarifa juu ya Manji kutaka kugombea nafasi hiyo japo mwenyewe bado hajathibitisha, ingawa kitendo chake cha leo kimezidi kuupa nguvu uvumi wa kwamba anataka kugombea nafasi ya kuwa bosi wa Yanga.

Wakati huo huo taarifa nyingine zinasema kuwa mjumbe Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb naye muda wowote kutoka sasa atandoka makao ya Yanga kwa ajili ya kuchukua fomu za kugombea umakamu mwenyekiti.

Mwanachama mwingine maarufu wa klabu hiyo Issac Mazwaile naye ameshachukua fomu za kugombea nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji.(Na Elicy Michael)

Friday, June 1, 2012

EURO 2012:

KUTOKA KWA PLATINI MPAKA DAVID VILLA: WATU SABA WALIOITAWALA MICHUANO YA EURO
Mastaa wengi wamewahi kung'ara kwenye michuano ya Ulaya - lakini ni wachache wameweza kutawala kama majembe haya.

Huku michuano ya nchini Poland na Ukraine ikiwa karibuni kuanza, tunachukua nafasi hii kukuletea watu saba ambao waliwasha moto wa kutisha kwenye historia ya michuano ya Euro.

MICHEL PLATINI (1984)
Mfaransa huyu  kwa sasa anajulikana zaidi kama Raisi wa Uefa mwenye sheria za utata zaidi, lakini hakuna mchezaji aliyeitawala michuano ya 1984 kama yeye.

Kiungo huyu wa aina yake alifunga mabao tisa kwenye mechi tano huku akiiongoza nchi yake kushinda ubingwa wa ulaya kwenye ardhi ya nyumbani.

Baada ya kufunga hat-tricks mbili kwenye mechi za hatua ya makundi, Platini alifunga bao kwenye dakika za nyongeza za mechi ya nusu fainali dhidi ya Ureno.

Ufaransa wakaingia fainali na kwa mara nyingine alifanya balaa kwa kupiga faulo iliyotinga nyavuni kwa kumshinda golikipa wa Spain Luis Arconada.

MARCO VAN BASTEN (1988)

 Career ya Mholanzi iliishia njiani kutokana na balaa la majeruhi, lakini huyu jamaa alikuwa kwenye kiwango cha juu sana.

Unless, labda kama ulikuwa muingereza, baada ya timu zote mbili za mataifa haya kufungwa kwenye mechi zao za ufunguzi, mechi ya kundi B kati ya Uholanzi na England ilikuwa muhimu sana.

Van Basten akafunga hat-trickna kumsumbua sana kinda Tony Adams, wakati wadachi walipowafungasha virago England.

Mchezaji bora wa ulaya kwa mara ya tatu alienda na kufunga goli la ushindi la ushindi dhidi ya Ujerumani magharibi kwenye nusu fainali lakini balaa zaidi lilikuwa njiani.

Van alifunga bonge la bao kwenye 'impossible angle' dhidi ya Umoja wa Soviet - goli ambalo linatajwa kama moja ya mabao bora kabisa ya fainali za ulaya.

Alimaliza michuano hiyo kama mfungaji bora.
PETER SCHMEICHEL (1992)
Ulikuwa umepita mwaka mmoja tu tangu Sir Alex Ferguson alipe £505,000 kumnunua mdenmark huyu.

Denmark haikuwa hata ikitakiwa kushiriki michuano hiyo lakini walichukua nafasi ya nchi iliyokuwa kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe Yugoslavia na wakaweza kuwashangaza watu na kubeba ndoo ya ulaya.

Hilo liliwezekana zaidi kutokana na uwezo wa golikipa ambaye alitisha sana kwa kuzuia michomo ya hatari.

Schmeichel aliikoa mpaka penati ya Marco van Basten na kupelekea Uholanzi iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa kutolewa kwenye mashindano katika hatua ya nusu fainali.

Hatari ya Denmark iliendelea huku Schmeichel akitoka na clean sheet kwenye ushindi wa 2-0 kwenye fainali dhidi ya Ujerumani.

ALAN SHEARER (1996)
Kwa kukumbuka kiangazi cha mwaka 1996, mshambuliaji huyu alikuwa akiwafanyia umafia mabeki wa pinzani    - akifunga magoli kutoka kwenye kila angle - alikuwa mshambuliaji wa kati aliyekamilika haswa.

Ndio ni rahisi kusahau kwamba alienda kwenye Euro 96 akiwa hajafunga katika mechi 12 ndani ya 21 akiwa na England.

Ingawa makelele yote aliyokuwa anapigiwa kocha Terry Venables kumtema mshambuliaji yalianza kuisha na kusahaulika mara tu alipofunga goli kwanza kwenye michuano hiyo katika dakika ya 22 dhidi ya Switzerland.

Kutoka pale akaendeleza balaa zaidi. Kwenye mechi dhidi ya Scotland na kabla ya kuwatesa sana Uholanzi kwenye mechi ambayo England iliwakandamiza wadachi 4-1 pale Wembley.

Shearer aliendeleza kufunga mabao katika mechi robo fainali England ikiwatoa Spain kabla ya kuwapa mashabiki wa England mwanzo mzuri alipofunga bao la kuongoza dhidi ya Ujerumani, ingawa England wakatolewa kwa mikwaju ya penati baada ya Gareth Southgate kukosa penati yake.

Shearer alimaliza michuano hiyo kama mfungaji bora na kubeba kiatu cha dhahabu.


ZINEDINE ZIDANE         
Wakati mwingine wa dhahabu wa michuano hii kwa Ufaransa ulihitimishwa na David Trezeguet.
Lakini wakitoka kushinda kombe la dunia miaka miwili nyuma, michuano hiyo iliyofanyika kwenye ardhi za Uholanzi na Ubelgiji ilimpa nafasi Zidane nafasi ya kuweka heshima zaidi kwamba ndio mchezaji bora wa wakati wake.

Wakisikia kelele za mwangi za ushindi wa akina Platini miaka 16 nyuma, Zidane akafunga bao kwenye extra time dhidi ya Ureno katika nusu fainali ya aina yake - kwa mkwaju wa penati.

Zidane alikuwa akitimiza miaka 30 siku tisa kabla ya fainali na akapokea zawadi ya siku ya kuzaliwa kwa kutajwa na UEFA kama mchezaji bora wa michuano hiyo.



OTTO REHHAGEL (2004)

Shujaa aliyekuwa hategemewi, mjerumani, ambaye sasa ana miaka 73, akawa mungu wa soka nchini Ugiriki  baada ya kuiongoza nchi hiyo kwenye kubeba kombe mwaka 2004

Akiwa bingwa wa kuunda ukuta wa kupaki basi golini chini ya nahodha, Theo Zagorakis kutoka Leicester City, Rehhagel alifanya maajabu mwaka 2004.

Aliiongoza timu yake kupita kwenye hatua ya makundi huku wakishinda mechi zote kwa ushindi wa 1-0 - hata ushindi wa fainali dhidi ya Ureno ulikuwa wa goli 1-0 dhidi ya wenyeji.

Siri ya mafanikio? Nyuma ya kila kocha aliyefanikiwa kuna mke mzuri wa kocha huyo na mama watoto wa Otto, Beate, ameripotiwa huwa anaenda kufanya scouting kwa wapinzani kwa ajili ya mumewe.

DAVID VILLA 2008
Ilikuwa ni michuano ambayo wahispania waliweka heshima baada ya kutaniwa kama warembaji kwa muda mrefu - lakini kipaji cha ajabu cha David Villa kiliiongoza Spain kujenga heshima mpya.

Mshambuliaji wa Valencia tayari alikuwa ameshafunga mabao 6 kwenye hatua ya kufuzu na akafungua michuano kwa kufunga hat-trick dhidi ya Russia.

Huku akiwa anamfunika patna wake mshambuliaji mpya wa Liverpool Fernando Torres, Villa then akafunga goli la muda wa majeruhi katika mchezo wa pili dhidi ya Sweden.

Alipumzishwa kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi, na akarudi kwenye robo fainali na akafunga bao la penati kwenye hatua ya mikwaju ya penati dhidi ya Italia na kuisadia timu yake kufika nusu fainali.

Alipata maumivu kwenye nusu fainali na akashindwa kupata nafuu kucheza mchezo dhidi ya Ujerumani ambao Fernando Torres akafunga bao la ushindi dhidi ya Ujerumani na kuwapa ubingwa Spain - huku David Villa akiibuka mfungaji bora wa michuano.

JE MWAKA HUU NANI ATAITAWALA  MICHUANO YA 2012.







EXCLUSIVE: KAPOMBE + JONAS + 50 MILIONI = IBRAHIM JEBA

Mauzauza kwenye soka la Bongo yameendelea kujidhihirisha leo.


Wakati klabu ya Simba ikiwa imejihakikishia kukamilisha usajili wa kinda la Azam under 20, Ibrahimu Jeba ambaye leo hii asubuhi alionekana kwenye mazoezi ya gym ya Simba - maeneo ya Chang'ombe. Uongozi wa klabu ya Azam FC umesema Simba inajidanganya kuhusu kumsajili mchezaji huyo ambaye Azam walimpeleka Villa Squad kwa mkopo kwa kujifua zaidi msimu uliopita.


Akizungumza na simu kutoka nchini Marekani meneja wa klabu ya Azam FC, Patrick Kahemele amesema mabingwa wa Tanzania bara wanafanya uhuni kwenye uhamisho wa mchezaji huyo ambaye bado ana mkataba na klabu hiyo inayomilikiwa na mfanyabiashara Salim Bakheresa. "Simba wanafanya uhuni katika hili kama ilivyo kawaida yao, Jeba ni mchezaji wetu halali na bado ana mkataba na Azam. Kumbukumbu sahihi nilizonazo ni kwamba Ibrahimu Jeba alisaini mkataba wa kuichezea Azam kwa miaka miwili mwezi Desemba 2011 na akachukua kiasi cha fedha kama ada ya usajili - kabla ya kuelekezwa kwamba akacheze Villa Squad kwa mkopo ili apate nafasi ya kujifua then msimu huu arudi Azam FC. Simba wakaenda wakamrubuni asicheze Villa, na Jeba bado mdogo hivyo ikawa rahisi kumrubuni, na Azam hatukutaka kufanya nao malumbano kwa sababu suala hilo tayari tuna mkataba ambao umesajiliwa kabisa na TFF, ambao walishatuambia haki zetu za msingi zitalindwa."


Kahemele alipoulizwa ikiwa Simba wanataka kulimaliza hilo suala itabidi walipe kiasi gani alijibu, "Kiukweli sie tulishatangaza mapema kwamba hakuna mchezaji yoyote ambaye ameachwa wala yupo sokoni kwa msimu ujao. Hivyo kama Simba wanamtaka Ibrahimu Jeba kihalali basi atawagharimu sana kwa kuwa sisi tunamuona Jeba akiwa na thamani ya Shilingi millioni 50 na uwachanganye wachezaji wawili wa Simba Jonas Mkude na Shomari Kapombe, then hapo tunaweza kuwafikiria kuwaachia Jeba vinginevyo haitowezekana Jeba kuichezea klabu yao."


HIKI NDIO KIKOSI RASMI CHA AZAM KWA AJILI YA MSIMU UJAO.
Kikosi Kamili cha Azam FC msimu ujao ni kama ifuatavyo Magolikipa ni Mwadini Ally, Deo Munishi "Dida" Aishi Salum na Jackson Wandwi
Mabeki wa Pembeni kulia ni Ibrahim Shikanda na Erasto Nyoni na kushoto ni Waziri Salum na Samih Haji Nuhu
Babeki wa kati ni Luckson Kakolaki, Said Moradi, Joseph Owino na Aggrey Morris
Viongo ni Kipre Bolou, Abdulhalim Humud, Himid Mao, Salum Abubakar, Abdi Kassim Sadala, Ramadhani Selemani Chombo, Abdulghani Ghulam, Ibrahim Rajab Jeba, Jabir Aziz Stima, na Ibrahim Joel Mwaipopo
Washambuliaji wa pembeni ni Kipre Tchetche, Mrisho Ngasa, Zahoro Pazi, Khamis Mcha, na George Odhiambo "Blackberry" Washambuliaji wa kati ni Gaudence Mwaikimba na mchezaji bora wa Azam FC John Raphael Bocco "Adebayor" (Na Elicy Michael)

EXCLUSIVE:

TAIFA STARS WAKIWA KWENYE MAZOEZI JIJINI ABDIJAN
Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa 'Kilimanjaro Taifa Stars' wakiwa kwenye
mazoezi ya viungo
Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa 'Kilimanjaro Taufa Stars' wakiwa kwenye
mazoezi chini ya Kocha Msaidizi Sylvester Marsh.
Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa 'Kilimanjaro Taifa Stars' wakiwa kwenye
mazoezi ya viungo chini ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen.

 Juma Nyosso na John Bocco wakipambana kwenye mazoezi.
Kipa wa timu ya soka ya Taifa 'Kilimanjaro Taifa Stars' akiwa kwenye
mazoezi ya viungo
Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa 'Kilimanjaro Taifa Stars' wakiwa kwenye
mazoezi ya viungo chini ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen:(Na Elicy Michael Abdijan)


HADHARA CHARLES AUNGANA NA KINA NWANKWO KANU NA PATRICK MBOMA KWENYE KAMPENI YA ' PLAY FOR THE UNION '





 Hadhara akifanya vitu vyake kwenye mitaa ya jiji la YOUNDE,nchini Cameroon.







  Hawa ni Baadhi ya washiriki wa Kampeni ya PLAY FOR THE UNION, Kampeni ambayo mabalozi wake ni Wanasoka wa zamani wa kulipwa Nwanko Kanu kutoka nchini Nigeria pamoja na Mshambuliaji Patrick Mboma toka nchini Cameroon.

AZAM FC YAZINDUA JEZI YA MSIMU UJAO





HIZI NDO JEZI ZITAKAZOTUMIWA NA AZAM FC MSIMU WA 2012-2013.

HIZI NDO JEZI ZITAKAZOTUMIWA NA AZAM FC MSIMU WA 2012-2013.