Wednesday, May 23, 2012

BAADA YA BOBAN KUANGUKA NA KUZIMIA - DAKTARI ASHAURI WACHEZAJI WA SIMBA KUPEWA TIBA YA SAIKOLOJIA





Baada ya Haruna Moshi kuzimia kwenye Uwanja wa Ndege wa Kinshasa juzi,  Daktari wa Timu ya Taifa 'Taifa Stars', Mwanandi Mwankemwa amesema wanawapa ushauri wa karibu wachezaji wa Simba waliopo katika timu hiyo ili warejee katika hali zao za kawaida.

Haruna 'Boban' presha yake ilishuka ghafla Jumatatu asubuhi alipokuwa Uwanja wa Ndege wa Kinshasa na kulazimika kupatiwa huduma  haraka na daktari wa uwanjani hapo kwa zaidi ya saa 1:30.

Daktari aliyemtibu, alimpa kahawa na chumvi na alimshauri asifikirie mambo mengi wala kufanya kazi ngumu kwa vile presha yake itashuka na kugharimu maisha yake.

Dk Mwankemwa alisema tukio la kifo cha ghafla cha Patrick Mafisango haliwezi kusahaulika mapema kwa wachezaji wenzake, na kwa sababu hiyo wanahitaji uangalizi wa karibu kiushauri ili kuhakikisha wanarejea kwenye hali yao ya kawaida.

Alisema kuna athari kubwa kwa mchezaji kucheza uwanjani huku akikosa utulivu wa akili kichwani kutokana na msongo wa mawazo juu ya tukio lolote la kusikitisha linaloweza kumgusa kwa karibu.

"Ni rahisi hata mchezaji kuumia anapocheza uwanjani, huku akili yake ikijaa kumbukumbu ya tukio baya kama ajali iliyosababisha kifo cha Mafisango," alisema Mwankemwa.

Daktari huyo alisema zaidi kuwa, ili mchezaji aweze kushiriki vizuri kwenye mchezo ni lazima aingie uwanjani akili yake ikiwa imetulia bila kuwa na msongo wa mawazo kwa jambo lolote lile.

"Kwa maana hiyo, tunachofanya kwa sasa ni kuwapa ushauri kila wakati ili kuwaondoa katika hali, tunatarajia hali itakuwa nzuri baada ya siku kadhaa, ingawa mwisho wa siku mwalimu wao (Kocha Kim Poulsen) ataamua ni wachezaji gani anaweza kuwatumia," alisema Mwankemwa ambaye pia ni daktari wa timu ya Azam FC.

Kauli ya kocha huyo imekuja siku chache tangu kiungo wa Simba, Moshi 'Boban' aliyeonekana kuguswa zaidi na kifo cha Mafisango kupata matatizo ya kiafya muda mfupi baada ya kushiriki mazishi Jumapili iliyopita.

Mchezaji huyo wa Simba tangu alipopokea taarifa ya kifo cha Mafisango alikuwa hawezi kuzungumza lolote zaidi ya kububujikwa na machozi ya uchungu, jambo ambalo linaweza pia kumwathiri kiuchezaji.

Boban ni miongoni mwa wachezaji walioitwa na Kocha Kim Poulsen kuunda kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kinachojiandaa na mchezo wa ugenini dhidi ya Ivory Coast kuwania tiketi ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia.Na Elicy Michael

AZAM KWENYE MICHUANO YA KAGAME KWA MARA YA KWANZA MWAKA HUU





WASHINDI wa Medali ya Fedha ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC watashiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame Julai, mwaka huu, Dar es Salaam, imeelezwa.
Kuingia kwa Azam kwenye michuano hiyo, iliyofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1974, kunamaanisha Tanzania Bara, wenyeji watawakilishwa na timu tatu, nyingine zikiwa ni mabingwa watetezi wa Kombe hilo, Yanga na mabingwa wa Ligi Kuu, Simba SC.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah Malabeja amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba maandalizi ya michuano hiyo, yanaendelea vizuri na tayari wadhamini wamekwishapatikana na watatangazwa katika Mkutano maalum hivi karibuni.  Na Elicy Michael

PATRICK MAFISANGO KUAGWA KESHO LEADERS CLUB ASUBUHI







Hatimaye kesho wapenzi wa soka nchini watapata kuuaga mwili wa marehemu Patrick Mafisango aliyefariki leo alfajiri wakati akitoka klabu na wenzie wanne, ataagwa kesho asubuhi katika viwanja vya leaders club kinondoni - jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa meneja wa Simba Nico Nyagawa - Mwili wa Mafisango baada ya kuagwa utaondoka na kusafirishwa na ndege ya shirika la KQ kuelekea kwao Rwanda kwa ajili ya mazishi.

Nyagawa amewaomba wapenzi wote wa Simba na soka kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kumuaga kipenzi chao, mchezaji ambaye enzi za uhai wake alitoa mchango mkubwa katika kuisadia Simba kupata mafanikio waliyoyapata msimu huu.


Mafisango aliyekuja nchini mwaka juzi na kujiunga na Azam kabla ya kuhamia Simba mwaka jana, alizaliwa Machi 7, mwaka 1987 mjini Kinshasa, DRC alikoanzia soka kabla ya kuhamia Rwanda, ambako baadaye alichukua uraia wa nchi hiyo.
Kabla ya kuja Tanzania alichezea APR ya Rwanda. Mechi ya mwisho Mafisango kuichezea Simba ilikuwa dhidi ya Al Ahly Shandy nchini Sudan Jumapili katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, ambayo Simba ilitolewa kwa penalti 9-8, kufuatia sare ya jumla ya 3-3.
Hadi anafariki dunia, Mafisango alikuwa ni tegemeo Simba katika safu ya kiungo na jana tu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nange 'Kaburu' alisema kiungo huyo yupo kwenye mpango wa kocha wa kikosi cha msimu ujao. 
Pamoja na kucheza kama kiungo, Mafisango pia anamudu kucheza nafasi ya beki wa kushoto na beki wa kati.
Japokuwa alikuwa kiungo, lakini pia alikuwa hodari wa kufunga mabao na msimu huu imeshuhudiwa akiifungia Simba mabao 11 katika Ligi Kuu na manne kwenye Kombe la Shirikisho.Na Elicy Michael

HII NDIO GARI ILIYOCHUKUA UHAI WA KIPENZI CHETU MAFISANGO - WENZAKE WANNE WANASURIKA

HII NDIO GARI ILIYOCHUKUA UHAI WA KIPENZI CHETU MAFISANGO - WENZAKE WANNE WANASURIKA:


Ndugu yake Mafisango aliekua nae wakati wa ajali amesema Mafisango alifariki dunia hapohapo kwenye ajali wakati wakitoka Club kuelekea nyumbani, walipofika kwenye taa za barabarani Tazara Dar es salaam, Mafisango ambae ndio alikua anaendesha alijaribu kuziwahi taa lakini ghafla akakutana na mwendesha guta ambapo katika kumkwepa gari ilimshinda na kuingia mtaroni leo Alfajiri.

Alikua na wenzake watano kwenye gari ambapo wengine wanne wamepona japoa walipata majeraha madogo madogo akiwemo mdogo wake ambae amesajiliwa na club ya Simba.

Haruna Niyonzima mchezaji wa Yanga alikua mchezaji wa mwisho kubadilishana jezi na Mafisango Tanzania, katika mechi ambayo Mafisango alifunga goli lake la mwisho.

Anasema Ijumaa ndio Mafisango alimwambia atasafiri kwenda Rwanda kujiunga na kikosi cha timu ya taifa, hili ni pigo kwa Tanzania, Rwanda na hata Congo DRC.

Na Elicy Michael

Friday, May 11, 2012

Washindi wa Tuzo za Mziki za Kili 2012 waitikisa Mwanza

Mkali wa Bongo fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond akiimba jukwaani hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award iliyofanyika uwanja wa Kirumba jijini Mwanza.

 Barnaba Boy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume akimbo jukwaani hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Mwanza katika Uwanja wa Kirumba.

  Msanii AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani na wacheza sho wake wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Mwanza katika Uwanja wa Kirumba .
 Barnaba akipiga picha kwa staili yake.

Diamond akiwa juu katika machuma ya Jukwaa.
 Vijana wa Kazi wa Diamond wakiwajibika .
 Roma Mkatoli akishusha mistari.
Msanii AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani.
 Isha Mashauzi akifanya vitu vyake.
Ben Paul nae akikimbiza .
Omy Dimpoz nae alifanya vitu vyake.
DJ Choka akimsindikiza Roma Mkatoliki.
 Mashabiki wakifuatilia show kwa furaha zaidi ndani ya kirumba hall.
 Huyu ni Diamond wa Mwanza akiongoza show ya mashabiki wake.
Mashabiki walifurika wakifurahia tamasha kwa hisia zao.

**********************************************************************************
******
WASANII wa Musiki wa Kizazi Kipya Diamond, Roma, Isha Mashauzi, AT, Barnaba, Omy Dimpoz, Ben Paul wamefunika vibaya katika Tamasha la Kili Music Award Winners Tour lililofanyika katika Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza, na kutoa burudani ya uhakika kwa wapenzi wa burudani ya Musiki wa jiji hilo na vitongoji vyake.

Show hiyo kali iliyoanza majira ya saa 8 mchana ikitanguliwa na makundi kadhaa ya wasanii chipukizi wa Bongo Fleva wa Jijini Mwanza ilizidi kupamba moto muda hadi muda hadi pale wasanii Nguli na washindi wa Tuzo za Kili Music Award 2012 walkipowasili uwanjani hapo.

Katika kukuza vipaji na kuibua vipaji vipya vya wasanii chipikizi Msanii Christian Joachim maarufu kama Christian JJ alifanikiwa kuwashinda wenzake wawili akiwepo mwana dada kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino cha Jijini Mwanza Bertha Denis.

Christian JJ aliibuka kidedea baada ya kupata kura nyingi za mayowe zilizo lipuka kutoka kwa mashabiki takribani wote uwanjani hapo na kuungana na mshindi mwingine kutoka mkoani Dodoma ambao wataenda jijini Dar es Salaam kurekodi nyimbo yao moja kwa Mtayarishaji wa Muziki maarufu.

Alianza jukwaani kupanda mwanadada wa Kikurya anaeimba Taarabu, Isha Mashauzi wa Mashauzi Clasic ambaye alijinyakulia Tuzo ya Wimbo bora wa taarabu kupitia wimbo wa Nani kama Mama na kukonga nyoyo za wapenzi wa taarabu vilivyo kwa kuimba vibao vyake kadhaa.

Isha Mashauzi alifuatiwa Jukwaani na mshindi wa Tuzo ya wimbo Bora wa R&B.
Msanii Ben Paul ambaye alijinyakulia tuzo hiyo kupitia kibao Number One ambapo nae alishambulia jukwaa vilivyo.

Omy Dimpoz alifuata jukwaani kwa kuimba nyimbo zake kadhaa ikiwapo ile iliyo mpa tuzo ya Wimbo bora wa Kushirikishwa ya Nai Nain a kusindikizwa na wacheza show wake wanne.

Mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji bora wa Kiume, Barnaba alifuata jukwaani na kuimba nyimbo kadhaa na kumpisha Mkali kutoka Zanzibar ambaye ni mshindi wa Tuzo Wimbo Bora wenye Vionjo vya Kiasili AT ambaye aliimba nyimbo kadhaa ikiwepo iliyompa Tuzo ya Vifuu Utundi amabyo aliicheza vilivyo na wanenguaji wake waili wa kike.

Baada ya Kushika AT alipanda tena Barnaba kasha kumpisha Mkali wa Tuzo za Kili Music Award 2012 Diamond ambaye alijizolea Tuzo tatu alipanda jukwaani kwa kishondo huku akiwatanguliza wacheza show wake.

Diamond akishangiliwa vilivyo aliimba sambamba na kucheza nyimbo zake takriban zote huku zilizo mpa tuzo za Wimbo Bora wa Mwaka na ule wa Mawazo uliompa Tuzo bora ya Video bora zikishangiliwa vilivyo.

Diamond ambaye ndiye anazungumzwa kwa sasa kuwa msanii ghali na bora nchini alimudu vyema kushambulia jukwaa na kuwafanya mashabiki muda wote mikono kuwa hewani.

Pazia la Wasanii washindi wa tuzo za Kili Music Award 2012 wanaofabnya ziara na waliobahatika kufika jijini Mwanza lilifungwa na Roma Mkatoliki a.k.a Mpare wa milimani aliyeshambulia jukwaa kwa nyimbo zake kadhaa za mistaari ya maandiko.

Roma ambaye ni Mshindi wa tuzo mbili za Wimbo Bora wa Hip Hop kupitia wimbo wake wa Mathematics na Tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop, alishambulia jukwaa huku viitikio vyake vikiimbwa na DJ Choka.

Wasanii hao wiki ijayo wanataraji kutoa burudani kama hiyo Mkoani Kilimajaro katika mji wa Moshi na tayari walisha tumbuiza na kuwashukuru mashabiki wao wa Mkoani Dodoma kwa kuwapa kura za ushindi.Na ELICY MICHAEL

KALI YA LEO:

KALI YA LEO: BOBAN ASAFIRI KWENDA SUDAN AKIVAA KANDAMBILI
                                      Haruna Moshi Boban akiwa ndani ya kandambili uwanja wa taifa jana.


Kiungo mshambuliaji wa timu ya Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ jana alikuwa kivutio kwa mashabiki, wasindikizaji na hata baadhi ya wasafiri waliomuona wakati wakiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, kuelekea Sudan.
     Simba inakwenda Sudan katika mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahli Shendi utakaopigwa Jumapili, huku ikiwa na mtaji wa ushindi wa mabao 3-0, iliyoupata kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Uvaaji wa Boban, ndio uliowavutia watu kumtizama, kutokana na kuvaa kama mtu asiyesafiri.
   Boban alikuwa amevaa fulana, suruali ya kimichezo ‘trakisuti’ na kandambili, hivyo kusababisha watu kuvutika kumuangalia, huku baadhi yao wakibaki kujiuliza kuhusu vituko vya nyota huyo ambaye mashabiki humuita Balotteli wa Bongo.
 Mchezaji huyo anafananishwa na mshambuliaji mahiri wa Italia, anayekipiga klabu ya Manchester City ya England, ambako mara kwa mara amekuwa akibeba vichwa vya habari katika magazeti ya England na Ulaya kutokana na vituko vyake.
Ukiondoa vituko hivyo vya uvaaji wa Boban, msafara wa watu 25 wakiwamo viongozi watano na wachezaji 20 wa timu hiyo waliondoka chini ya uongozi wa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Hussein Mwamba, majira ya saa 10:00 Jioni.Na Elicy Michael..

Thursday, May 10, 2012

RADEMEL FALCAO NI HATARI: AIONGOZA ATLETICO MADRID KUTWAA UBINGWA WA EUROPA CUP.

RADEMEL FALCAO NI HATARI: AIONGOZA ATLETICO MADRID KUTWAA NDOO YA EUROPA KWA KUWATANDIKA WABABE WA MAN UNITED 3-0

Na Elicy Michael.

Wednesday, May 9, 2012

TANZANIA YAICHAPA LESOTHO 57-13 MICHUANO YA AFRIKA YA NETIBOLI

Kikosi cha timu ya Taifa ya Lesotho.




Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akisalimiana na wachezaji wa timu ya Taifa ya Netiboli ya Tanzania 'Taifa Queens'wakati ufunguzi wa mashindano ya Afrika yaliyoanza leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo Tanzania imeichapa Lesotho kwa 57-13

Wanamuziki wa Bendi ya Mwenge Jazz wakitumbuiza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Afrika ya Netiboli.


 Mlinzi wa timu ya taifa ya Netiboli Tanzania, ‘Taifa Queens’, Lilian Sylidion (kushoto), akiwania mpira mbele ya wachezaji wa timu ya Lesotho katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Afrika uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Taifa Queen's imeshinda 57-13.

 Kikosi cha Taifa Queen's.  Na Elicy Michael

Redd's Miss IFM zapamba moto

Mbio za Kumsaka Redd's Miss IFM zapamba moto.

 Warembo watakaoshiriki kinyang'anyiro cha kumsaka Redd's Miss IFM 2012 wakiwa kwenye pozi la picha jioni ya leo kwenye ukumbi wa Break Point,Posta jijini Dar es Salaam,ikiwa ni maandalizi ya Shindano hilo linalotarajia kufanyika Mei 12,2012 katika viwanja vya ufukwe wa Cine Club jijini Dar.

Mwalim wa Warembo hao wanaojiandaa na shindano la Redd's Miss IFM,Ester Willson (kushoto) akitoa somo kwa washiriki hao wakati wa mazoezi ya kujiandaa na shindano hilo.

Picha ya pamoja na Mwalim(Mkufunzi ) wao.Picha na Elicy Michael

JANGWANI KWAFUKUTA HAKUNA KUSIKILIZANA KWA TIMU.

WAZEE WA YANGA WATOBOA UKWELI KUHUSU 5-0 ZA SIMBA: DENI LA PAPIC NA WACHEZAJI ZAIDI YA MILIONI 75 NDIO CHANZO KIKUBWA CHA KIPIGO DHIDI YA  SIMBA.

Takribani zaidi ya masaa 48 baada ya klabu bingwa ya Tanzania bara na mwakilishi pekee wa Afrika mashariki na kati katika michuano ya kimataifa - Simba Sports Club kuifanyia mauaji ya kutisha mahasimu wao wa jadi klabu bingwa ya Afrika mashariki na kati Dar Young African kwa kuitandika bao tano kwa nunge - leo hii wazee wa klabu ya Yanga chini ya uongozi wa Ibrahimu Akilimali umeamua kuweka wazi sababu kuu zilizochangia mno kupokea kipigo kutoka kwa mnyama.

Akizungumza leo hii katika mkutano wa waandishi wa habari Mzee Akilimali kwanza kabisa alikana madai ya uongozi wa Mwanasheria Lloyd Nchunga kwamba wazee hao waliihujumu klabu hiyo katika mchezo, pia akimuonya Nchunga asithubutu kumfukuza mchezaji hata mmoja kwa madai ya kuhusika kuihujumu Yanga.

Mzee Akilimali pia amesema Nchunga na uongozi wake ndio watu wa kulaumiwa kwa klabu hiyo kupokea kipigo cha aibu kutoka kwa watani wao, huku akitoa sababu zifuatazo.

1: MAANDALIZI
Timu ya Yanga iliingia kambini siku tatu kabla ya mchezo dhidi ya Simba huku wachezaji wakiwa hawana morali yoyote kutokana na kuwa walikuwa wakidai malimbikizo ya mishahara na bonasi za mechi za msimu mzima.

2: KOCHA PAPIC NA MADAI YA MIL. 24
Kwa muda mrefu kocha mkuu wa Yanga amekuwa akiudai uongozi wa Yanga shilingi milioni 24 za malimbikizo ya mshahara wake, hali iliyopelekea Mserbia huyo kutokuweza kuishi vizuri nchini na kupelekea kutokuwa na maelewano mazuri ya uongozi hivyo mwishowe kukosa kabisa utulivu wa akili wa kuweza kuitumika klabu kuelekea katika crucial moment ya msimu-hasa katika mechi ya marejeano na watani wao jadi.

3: MADAI YA BONASI ZA  SHILINGI 70,000 KWA KILA MCHEZAJI KWA MECHI - MSIMU MZIMA. (JUMLA YA PESA ZA BONASI ZA MSIMU MZIMA NI 52,780,000)
Uongozi wa Yanga umejiwekea utaratibu wa kutoa bonasi ya shilingi 70,000 kwa kila mchezaji kila baada ya mechi. Lakini katika hali ya kushangaza ndani ya kipindi chote cha Ligi kuu ya Tanzania bara uongozi wa bwana Lloyd Nchunga haukuwalipa hata shilingi ya bonasi za mechi zote za msimu wachezaji kama walivyokubaliana. Na pale alipoulizwa alikuwa akitoa ahadi tu.Kutokana na deni hili na kushindwa kutimiza ahadi Lloyd hakuwa hata akienda kuangalia kambi inaendaje wala kuwatia hamasa wachezaji kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jadi. Kiukweli hali ya kambi ilikuwa mbaya kifedha na kuwafanya wachezaji wa Yanga kutokuwa katika hali nzuri ya kiakili kuweza kuvaana na wapinzani wao bila kuambulia matokeo ya namna ile. Ilifikia hatua mpaka wachezaji wakaamua kwamba kabla ya mechi walipwe pesa zao au hawatoenda uwanjani kucheza na Simba - kitu ambacho kama wangekifanya wangeweza kushushwa daraja kama adhabu. Lakini wale wale watu ambao Bwana Lloyd amekuwa akiwatuhumu kwamba wanawarubuni wachezaji na pesa zao chafu ndio waliokuja kuokoa jahazi na kutoa kiasi cha shilingi 300,000 kwa kila mchezaji, ja,bo ambalo liliwafanya wachezaji kuingia uwanjani kucheza japo kwa shingo upande.
Sasa mchezaji akiwa kwenye hali waliyokuwa nayo wachezaji hawa halikuwa jambo la ajabu kuona wakiwa katika morali ya chini na kucheza ovyo kwenye mechi dhidi ya Simba." -Alisema Mzee Akilimali.

MASWALI
Ikiwa tuhuma hizi zilizotolewa na wazee wa Yanga ni kweli. Je ni wapi zilipokuwa zinaenda fedha nyingi zinazotolewa na mdhamini wa klabu hiyo Bia ya Kilimanjaro kila mwezi kwa madhumuni ya kulipa mishahara ya wachezaji, kocha na staffs wengine? Papic anadai mshahara wake.

Yanga ina chanzo kikubwa cha kukusanya mapato ya mlangoni tofauti na timu nyingi kwenye ligi kuu. Je yale mapato yote waliyokuwa wakiyakusanya ama kuyapata kutokana na viingilio vya mashabiki yamekwenda wapi kiasi cha kufikia kushindwa kuwalipa bonasi wachezaji?

Kwa undani zaidi wa stori hii sikiliza taarifa kutoka kwa wazee wa Yanga.
(Na Elicy Michael)

SIMBA KWENDA SUDAN NA NDEGE YA KUKODI






BAADA ya kumaliza Ligi Kuu bara kwa kishindo, Simba sasa inajipanga kwa safari ya kwenda Sudan kwa ajili ya mechi ya michuano ya kimataifa, na imepanga kuondoka kesho kwa ndege ya kukodi.

Simba iliifunga Yanga mabao 5-0 juzi katika mechi ya mwisho ya Ligi hiyo na hivyo kunogesha furaha za kutwaa ubingwa ilioutwaa tangu Ijumaa iliyopita.

Akizungumza Dar es Salaam jana, makamu mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange ‘Kaburu’ alisema kuwa timu yao itaondoka kesho kwa ndege ya kukodi kuelekea Sudan kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Kombe la shirikisho dhidi ya Al Ahly Shandy ya huko.

Katika mechi ya kwanza ya raundi ya tatu ya michuano hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa takriban wiki moja iliyopita, Simba ilishinda kwa mabao 3-0 na hivyo kuhitaji sare ama ushindi wa aina yoyote kwenye mechi hiyo ili kufuzu kwa hatua inayofuata.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amesema kuwa mafanikio ya
timu yao msimu huu yanatokana na ushirikiano mzuri kati ya uongozi wa sasa, uongozi uliopita na marafiki wa klabu hiyo ‘Friends of Simba’.

Rage akizungumza baada ya ushindi wa juzi dhidi ya Yanga, alisema kuwa mshikamano
uliokuwepo ndani ya klabu hiyo kwa sasa ndio siri ya mafanikio ya timu yao.

Alisema kuwa siku zote panapokosekana mshikamano madhubuti miongoni mwa wanachama wa klabu hiyo lazima timu yao inakuwa haifanyi vizuri, lakini kwa sasa kwa kuwa wako pamoja ndio maana mafanikio yanaonekana mapema kabisa.Picha na Elicy Michael

TANZANIA YAANZA KWA KISHINDO MASHINDANO YA NETIBOLI YA AFRIKA

Kikosi cha timu ya Lesotho.


Kikosi cha timu ya taifa ya Netiboli ya Tanzania 'Taifa Queen's.

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akikagua timu ya Lesotho.

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akikagua timu ya Taifa Queen's.

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete akikumbuka enzi zake wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo.

Mshike mshike katika mchezo huo wa Ufunguzi.

Mfungaji wa timu ya Taifa Queens, Mwanaid Hassan akitafuta mbinu za kumtoka mlinzi wa Lesotho, Tjabane.

Moja ya hekaheka katika lango la Lesotho.

Pili Peter akimiliki mpira.

Pili Peter wa Tanzania akiwania mpira huku akizongwa na mchezaji wa Lesotho.


Taifa Queen's wakipiga jaramba.


Waamuzi wa mchezo huo wakisalimiana na mgeni rasmi.


Mashabiki wakiwa makini  kabisa wakifuatilia mpambano wa timu yao.



TIMU ya taifa ya netiboli ya Tanzania, Taifa Queens, leo imeanza vema mashindano ya Afrika baada ya kuichapa timu ya Lesotho kwa magoli 57-13, katika mechi ya ufunguzi iliyorindima kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Taifa Queens ikiongozwa na wafungaji wake, Mwanaidi Hassan ‘Pereirra’ (GS) na Irene Elias (GA), ambao walikuwa wakiunganishwa vema na kiungo, Faraja Malaki (C), Evodia Kazinja (WA), na Restuta Boniface (WD), hadi robo ya kwanza inamalizika, walikuwa mbele kwa magoli 13-3.

Robo ya pili, Taifa Queens ilizidi kuchanua mbele ya mgeni rasmi, Mke wa Rais Kikwete, Mama Salma, ambapo hadi inamalizika walitoka na magoli 23-9 huku robo tatu wakimaliza kwa 40-13.

Robo ya nne, ukuta wa Taifa Queens uliokuwa chini ya Lilian Sylidion (GD), na Doritha Mbunda (GK), uliwabana vilivyo wafungaji wa Lesotho na hadi mchezo unamalizika, waliibuka kidedea kwa ushindi huo wa magoli 57-13.

Michuano hiyo inayoshirikisha nchi nane, inaendelea tena leo kwa mechi kati ya Botswana na Zambia, Malawi na Zimbabwe, huku wenyeji Tanzania wakitupa karata tena kwa Zambia.
Picha na Habari na Elicy Michael

Tuesday, May 8, 2012

KOCHA WA AZAM FC: STEWART HALL ASEMA RUSHWA NDIO KIKWAZO CHA MAENDELEO YA SOKA TANZANIA



KOCHA wa Azam, Stewart Hall amelia na wadau wa Simba na Yanga wanavyoipiga vita timu yake, ambayo imeibuka kuwa kigogo cha Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na Mwanaposti katika mahojiano maalumu, Hall anasema anashangazwa na mashabiki hasa wa Simba na Yanga kwa kuijengea chuki timu yake kutokana na kutishia ubabe wao.

Hall anaonya kuwa tabia ya wadau wa Simba na Yanga wanaotaka kuona ligi ya Tanzania ikitawaliwa na timu mbili zao tu kitu ambacho si sahihi kwa maendeleo ya soka.

"Timu hizi zimekuwepo kwa miaka mingi sana lakini nashangaa zimeshindwa kusaidia kukuza soka la Tanzania.

"Ninachokiona katika soka la Tanzania kinanisikitisha na kinachonikera zaidi wameingia watu makini wa Azam, ambao wameingiza fedha lakini wanapigwa vita," anasema Hall, ambaye ni raia wa Uingereza.

Anasema Watanzania wanapaswa kuruhusu ushindani na kutolea mfano Ligi Kuu Scotland inavyoshindaniwa na timu mbili tu za Rangers na Celtic na kufanya soka la sehemu hiyo kuwa chini.

Ligi Kuu Tanzania Bara
Hall anasema anafurahia timu yake kushika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa miaka chache tangu kuanzishwa kwake.

Anaeleza ni kitu kizuri kuona timu yake iliyoanzishwa mwaka 2004, imeipiku Yanga iliyoasisiwa katika miaka ya 1930.

Azam safari hii imenyakua nafasi ya pili na mwakani itashiriki katika mashindano ya Kombe la Shirikisho.

Hall anaonya Watanzania wanapaswa kubadilika kama kweli wanataka soka la nchi hii ibadilike.
Anasema kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linatakiwa kuwa makini katika kuendesha katika ligi hiyo.

Analalamikia vitendo vya rushwa kwenye ligi hiyo na viwango duni vya uchezeshaji miongoni mwa waamuzi.

Hall anaeleza kuwa anashangaa kuona rushwa na upangaji matokeo vinakubalika kama sehemu ya soka la Tanzania.

"Ni hatari kwa soka la nchi yenu kama mtakubali masuala ya upangaji matokeo," anasema Hall, ambaye timu yake ililazimika kurudiana na Mtibwa kwenye mzunguko wa pili baada ya mechi ya kwanza kukatizwa kutokana na makosa ya mwamuzi Rashid Msangi.

Pia mechi za Yanga na Polisi Dodoma zilimalizika kwa waamuzi kupigwa kutokana na timu hizo kudai mwamuzi alikuwa anaibeba Azam.

Kocha huyo anakanusha vikali madai hayo na kudai kuwa watu wanaionea wivu tu timu yake kutokana na kuwa na fedha nyingi.

Hall anasema TFF kwa kushirikiana na wadau wa soka la Tanzania wanapaswa kupiga vita kwa nguvu zote masuala ya rushwa.

Anatahadharisha ni ndoto kwa timu za Tanzania kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa kama wadau wa soka watakumbatia rushwa kama sehemu ya soka la Tanzania.

Anasema wapangaji matokeo wanapaswa kuchukua hatua kali kama Marseille ya Ufaransa ilivyoadhibiwa mwaka 1993 baada ya kubainika ilikuwa inanunua baadhi ya mechi za Ligi Kuu Ufaransa au ile kashfa ya upangaji matokeo ya Italia iliyokuja kujulikana kwa jina la Calciopoli.

Anaonyesha kuwa ubaya wa timu kununua mechi unasababisha Tanzania kuwakilishwa na timu dhaifu kwenye michuano ya Afrika.

"Bwana mwandishi jiulize, timu gani ya Tanzania imetwaa kutwaa taji la Afrika? Jibu linafahamika na ni wazi kuwa linasababishwa na rushwa ndani ya Ligi Kuu," anaeleza Hall, ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Birmingham.

Hall, hata hivyo, anadai anategemea ushindani mkali zaidi msimu ujao kwenye Ligi Kuu kwani ameona timu kama Mtibwa na Coastal Union ziko juu.

Mashabiki wa Simba na Yanga
Hall anaeleza pia mashabiki wa Simba na Yanga kwa kiasi kikubwa nao wanachangia kwa kiasi kikubwa kuvuruga soka la Tanzania.

Anasema mashabiki hao wanaweka presha kubwa kwa wachezaji na viongozi wa soka kuhakikisha timu zao zinashinda.

Hall anatolea mfano vurugu za mechi ya Yanga na Azam kuwa zilichangiwa zaidi na viongozi na mashabiki wa Yanga kuwapa shinikizo wachezaji wao kushinda.

"Unajua tulikuwa tumeifunga Yanga mara kadhaa, sasa safari hii wakaona hapana wanapaswa kushinda kwa njia zozote. Basi baada ya kuona mambo hayaendi vizuri wakampiga mwamuzi," anasema Hall, ambaye pia ni Mshauri wa Ufundi wa timu ya Zanzibar.

Hall anasema anaelewa mashabiki wa soka wa Tanzania wamegawanyika kushabikia timu hizo lakini amesema zinapaswa kubadilika.

Anaeleza mashabiki wa timu hizo wanapaswa kuhakikisha timu zao zinaendeshwa kisasa zaidi ndani na nje ya uwanja badala ya kuendekeza siasa za nje ya uwanja.

Hall anaeleza kutokana na presha na wingi wa mashabiki wa Simba na Yanga kumefanya wababaike wanapochezesha mechi za baina ya timu hizo.

Pia ameponda mashabiki hao kwa kukosa uzalendo na kuzishabikia timu za kigeni zinapokuja kucheza Tanzania.

"Nimefundisha soka katika nchi mbalimbali duniani lakini sijawahi kuona timu ya kigeni inashabikiwa," anasema Hall.

Katika miaka ya karibuni, imekuwa kitu cha kawaida kwa mashabiki wa Simba na Yanga kushangilia timu za kigeni zinapocheza na mahasimu wao.

Hall anasema ameshangazwa kuwa tabia hiyo imeingia katika timu ya taifa.
"Mashabiki wa Simba na Yanga wanaua soka lenu kwani wameingiza siasa zao kwenye timu ya taifa," anaeleza Hall, ambaye alikuwa anazungumzia vituko vya Kombe la Chalenji mwaka jana wakati mashabiki wa Yanga walipokuwa wanaizomea timu ya Bara kutokana na kuwa na wachezaji wachache wa Yanga.

Pia anatolea mfano jinsi mashabiki hao walivyokuwa wanamsakama mshambuliaji wake John Boko na kumfanya ajitoe kwenye kikosi cha timu ya taifa.

"Boko ni mchezaji mdogo sana lakini ameacha kuchezea Stars kutokana na kujengewa chuki na mashabiki hawa. Watu hawa wanaua soka la Tanzania," anaeleza Hall.

Pia anaeleza kuwa mashabiki hao wamejenga chuki kubwa dhidi ya timu yake kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na matajiri wa timu hiyo.

Azam imejenga uwanja na hosteli ya wachezaji na ina mfumo mzuri wa timu kuanzia watoto wenye umri wa miaka 12.

Pia wachezaji wa timu hiyo wanaangaliwa vizuri kwa kulipwa mishahara na marupurupu kwa wakati.

"Mimi nilitegemea kuwa mashabiki hawa wangetuunga mkono na kushinikiza viongozi wao kubadilika na kuendesha timu zao vizuri lakini badala yake wanatupiga vita," anaeleza Hall kwa mshangao.

Hall anatoa mwito kwa wadau wa soka la Tanzania kuiangalia Azam kama kioo cha soka la Tanzania badala ya kuichukulia kama adui.

Maendeleo ya Azam
Hall anaeleza kuwa anasema licha ya changamoto za waamuzi lakini anapongeza timu yake kwa kushika nafasi ya pili nyuma ya Simba iliyotwaa ubingwa.

Amesema amefurahia kuona malengo yao yametimia msimu kwani walikuwa wanataka kuvunja ubabe wa Simba na Yanga kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

"Lengo letu kubwa lilikuwa kushika nafasi mbili za juu, kitu ambacho tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

"Sasa msimu ujao tunataka kupigania ubingwa jambo ambalo ninaamini tuna ubavu nalo," aliongeza Hall, ambaye amewahi kuzifundisha timu za taifa za St.Vincent, Grenada na Pune ya India.

Hall anafichua kuwa timu hiyo imeandaa programu ya miaka 10 yenye lengo la kuifanya timu hiyo kuwa miongoni mwa timu kubwa Afrika.

"Tunataka tufikie hatua kutoa upinzani kwa timu kama TP Mazembe au Al-Ahly ya Misri," anaongeza Hall.

Amesema kuwa anasikitishwa na kuona timu yake inapigwa vita na wadau wa soka.
Hall anasema kutokana na haya yanayowakuta Azam yatafanya watu wengine wenye fedha kuogopa kuingiza fedha zao kwenye soka.

"Unajua kuna watu wanaangalia tunayofanya sasa watu wenye fedha zao wakishuhudia jinsi Azam inavyonyanyasika basi hawatataka kushiriki katika mchezo huu," anasema Hall, ambaye anaongeza fedha ni muhimu kwa maendeleo ya soka.
(By Elicy Michael)

MWANAMUZIKI WAKUNDI LA MAKOMA AJULIKANAE KWA JINA LA TUTALA MAKOMA ALIPOMTEMBELEA MH: VICKY KAMATA!

MWANAMUZIKI WAKUNDI LA MAKOMA AJULIKANAE KWA JINA LA TUTALA MAKOMA ALIPOMTEMBELEA MH: VICKY KAMATA!

Tutala Makoma alipomtembelea Mhe.Vicky Kamata nyumbani kwake na kulia ni Mr Gorge kutoka Praise Power na katikati ni Groly binti wa Vicky Kamata.

Tutala na Groly


Mhe. Kamata, Tutala na mrembo Groly katika Pozi (Na Elicy Michael)


SIMBA BINGWA VODACOM PREMIER LEAGUE 2012

SIMBA YAIKUNG'UTA YANGA GOLI 5-0 NA KUBEBA UBINGWA WA VODACOM PREMIER LEAGUE:

Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma baada ya timu ya Simba kuifunga Yanga magoli 5-0 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar salaam katika mchezo uliokuwa ni wa  kumaliza michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom uliomalizika jioni hii  kwenye uwanja wa Taifa, huku ikiwa tayari ni mabingwa wapya wa ligi hiyo, Simba imefanikiwa kutunza heshima yake baada ya kuifunga Yanga magoli 5 kupitia wachezaji wake Emmanuel Okwi, goli la kwanza.

Goli la pili la Simba likafungwa na mchezaji Felix Sunzu kwa njia ya penati na dakika chache baadae Emmanuel Okwi akaongeza goli la tatu , Juma Kaseja akaongeza goli la nne kwa penati wakati pia Patrick Mafisango akafunga hesabu kwa kufunga  goli la tano baada ya wachezaji wa Yanga kufanya makosa katika eneo la hatari.

Mchezaji wa timu ya Simba mganda Emmanuel Okwi akishangilia goli mara baada ya kuifungia timu yake goli la kuongoza.

 Wachezaji wa Simba wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe  leo kwenye uwanja wa Taifa.

Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimvisha Medali mtoto wa mchezaji Uhuru Selemani wa Simba.

Waziri wa Habazri, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk Fenela Mkangara akimvisha medali mshabuliaji wa Simba Emmanuel Okwi.

Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia na kocha wao kwa kumbeba juu juu.

Luninga kubwa ya uwanjani ikionyesha magoli yaliyofungwa na Simbaaa dume.

Mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi akiwania mpira mbele ya Shadrack Nsajigwa wa Yanga katika mchezao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania inayomalizika.

Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia timu yao.

Mashabiki wa timu ya Yanga wakiangalia kitu jukwaani haikufahamika lilikuwa ni tukio gani.

Wachezaji wa timu za Simba na Yanga wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.

Kikosi cha timu ya Simba ambao ndiyo mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom 2011-2012 kikiwa katika picha ya pamoja na Kocha wao Milovan.


Manahodha wa Simba na Yanga Juma Kaseja kushoto na Shadrack Nsajigwa wakisalimiana mbele ya waamuzi kabla ya kuanza kwa mpambano huo.

Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa wamefurika uwanjani hapo.

DK: 1 - Emmanuel Okwi wanawainua Simba vitini

Jukwaa la mashabiki wa yanga.


Mashabiki wa Simba Walivyofurika.



MWARI WA VPL AKISUBIRIWA KUKABIDHIWA KWA WANA WA MSIMBAZI ( Picha Zote na Elicy Michael)