UONGOZI MBOVU: GODFREY NYANGE KABURU AMSAJILI MCHEZAJI BILA KOCHA WALA KAMATI YA UFUNDI YA SIMBA KUJUA.
Moja ya chanzo kikubwa kinachookwamisha maendeleo ya soka la Tanzania ni kuwa na viongozi wasiojua mipaka ya madaraka na majukumu yao. Huu ni ugonjwa mkubwa unaolikabili soka la Tanzania hususani katika vilabu vikubwa nchini kwetu ambavyo kwa muda mrefu vimekuwa ndio uti wa mgongo wa soka letu - yaani Simba na Yanga.
Hili suala limeendelea kujidhihirisha leo pale ambapo kumetokea sintofahamu kati ya kamati ya ufundi ya klabu bingwa ya Tanzania Simba Sports Club na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo bwana Godfrey Nyange Kaburu baada ya bwana Kaburu kuamua kumsajili mshambuliaji kutoka klabu ya Ruvu Shooting Abdallah Juma bila kufuata taratibu za usajili ndani ya klabu zinavyojieleza na kupaswa kuwa.
Nyange bila kupata maoni ya kocha wala jopo zima la kamati ya ufundi leo hii amekamilisha usajili wa mchezaji huyo kwa maamuzi yake binafsi - jambo ambalo kamati nzima ya ufundi imeona na uingiliwaji wa majukumu alioufanya kiongozi huyu mkubwa wa Simba.
NO WONDER SOKA LA TANZANIA LIMEENDELEA KUDUMAA FOR THE LACK OF PROFESSIONALISM!!!!
(By Elicy Michael)
No comments:
Post a Comment