Tuesday, May 1, 2012

KASEJA awaonya wenzake kuhusu ushi.......


KIPA wa Simba, Juma Kaseja amewataka wachezaji wenzake kuzipotezea ndoto kwamba ushindi wa mabao 3-0 waliopata dhidi ya Al-Ahly Shendi, ni kama tayari wameshafuzu kwa hatua nane bora Kombe la Shirikisho.
Simba wanatarajia kurudiana na wapinzani wao wiki mbili baadaye nchini Sudan.Kaseja alisema ushindi huo unapaswa kutumika kama sehemu ya maandalizi ya mchezo ujao, na kamwe wasiidharau timu hiyo pamoja na kupoteza mchezo kwa idadi kubwa ya mabao.
"Siyo sahihi kudhani ushindi tuliopata dhidi Al-Ahly Shendi ni kama tayari umeshatuvusha kucheza hatua ya robo fainali.
"Binafsi, naamini matokeo ya mchezo wa marudiano ndiyo yatatoa picha halisi na siyo ushindi huu tuliopata nyumbani," alisema Kaseja.
Alieleza Al-Ahly Shendi ni timu nzuri na yenye wachezaji wenye uwezo mkubwa. "Nafikiri ulikuwa uwanjani umeona hilo na macho yako," aliongeza Kaseja.
by Vhttp://www.mwananchi.co.tz/michezo/16-kandanda/22511-kaseja-awaonya-wenzakeaileth Malile

No comments:

Post a Comment