KOCHA MPYA WA ENGLAND

Kocha mpya wa England Roy Hodgson ataongea na John Terry na Rio
Ferdinand kwa matumaini ya kuwachukua wachezaji wote wawili katika
michuano ya EURO 2012.
Kazi kubwa ya kwanza kwa Hodgson ni kunitibu majeraha ya uhusiano mbovu
uliopo baina ya wachezaji katika chumba cha kubadilishia nguo uliotokea
baada ya Terry kutuhumiwa kumtolea maneno ya kibaguzi Antoni Ferdinand -
ambaye ni mdogo wake Rio. mwezi October mwaka jana.
Terry na Ferdinand wanabakia kuwa mabeki wenye ushirikiano mzuri katika
timu ya taifa na wakati akitangazwa rasmi katika uwanja wa Wembley, Roy
alikaririwa akisema: "Itabidi niongee na John na Rio, natumaini
tutakutana uso kwa uso, na kujua nini suluhisho.
"Kwa sasa siwezi kusema chochote mpaka nitakapogundua kiundani
mahusiano yao yapoje - na nafikiri sitoongeea na wao tu, nitaongea na
wachezaji wote wakubwa ndani ya kikosi."
Hodgson, ambaye amesema kwamba atamchagua Wayne Rooney katika kikosi cha
wachezaji 23 - ambacho atakitangaza muda mfupi baada ya msimu kuisha -
bado hajaamua kuhusu wasaidizi wake.
Lakini inaaminika atamchagua msaidizi mmoja, ingawa bado hajaongea na
kocha wa England chini ya miaka 21 na kocha wa timu ya Uingereza ya
Olympic Staurt Pearce kuhusu jinsi ya kuhusika kwake katika EURO 2012.

Mtu anayetajwa sana kuweza kuchaguliwa kama msaidizi wa Roy ni Alan
Shearer ambaye anatajwa kuwa na mahusiano ya karibu sana na Hodgson.(Na Elicy Michael)
No comments:
Post a Comment